Polepole fuata sheria za kazi, saa 3 usiku siyo muda wa kazi

Polepole fuata sheria za kazi, saa 3 usiku siyo muda wa kazi

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Katibu mwenezi wa CCM na Mbunge wa kuteuliwa anaendesha kipindi mubashara cha "Papo Kwa Papo" saa 3 usiku lkn anawapigia simu watendaji wa serikali akitaka watolee ufafanuzi baadhi ya kero za wananchi.

Yaani anataka mambo ya kiofisi (ya kikazi) yatolewe ufafanuzi muda wa kukaa na familia ama kustarehe.

Anachokifanya mhe Polepole siyo udikteta?
Mbona anakiuka sheria na taratibu za kazi?

Watendaji wakitoa takwimu ama taarifa zinazokinzana watalaumiwa?
Wakigoma kupokea simu watendaji hawa watalaumiwa?
 
Unaacha Kuwaambia CHADEMA wako (hasa Kurugenzi yenu ya Habari) nao Wawe Wabunifu kama Wenzao wa CCM kwa kutumia kila Fursa katika Kujitangaza na kujiweka karibu hasa Kiimani na Kiitikadi za Kisiasa kwa 'Wafuasi' Wao, Wewe kilichopo Akilini mwako ni Majungu na Lawama tu pekee. Na ni Ubunifu kama huu anaofanya sana Polepole ndiyo unaing'arisha zaidi CCM na Kuaminika kwa Watu huku nyie mkilia lia kama 'Wehu' fulani vile.
 
Hizo kazi zenyewe kila wakati wanajisifu kuzichapa mbona hatuoni positive outcome kwa raia wa kawaida?!

Wanadhani kuongea sana na kuteka vyombo vyote vya habari ndio maendeleo ya nchi, wacha waendelee kujidanganya, wanajua fika hao watazamaji wameshawachoka.
 
Unaacha Kuwaambia CHADEMA wako (hasa Kurugenzi yenu ya Habari) nao Wawe Wabunifu kama Wenzao wa CCM kwa kutumia kila Fursa katika Kujitangaza na kujiweka karibu hasa Kiimani na Kiitikadi za Kisiasa Wewe kilichopo Akilini mwako ni Majungu na Lawama tu pekee. Na ni Ubunifu kama huu anaofanya sana Polepole ndiyo unaing'arisha zaidi CCM na Kuaminika kwa Watu huku nyie mkilia lia kama 'Wehu' fulani vile.
CCM ina aminika kwa nani?!

Mmeteka vyombo vyote vya habari halafu unajisifu huo ndio ubunifu?
 
Hizo kazi zenyewe kila wakati wanajisifu kuzichapa mbona hatuoni positive outcome kwa raia wa kawaida?!

Wanadhani kuongea sana na kuteka vyombo vyote vya habari ndio maendeleo ya nchi, wacha waendelee kujidanganya, wanajua fika hao watazamaji wameshawachoka.
2025 watabeba tena mabegi meusi yenye kura feki
 
Na hii weekend mtu unaweza kuwa upo mtungi au unavinjari maeneo na kimwana, mara unapigiwa simu utoe takwimu.
 
Back
Top Bottom