Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Dah mwendazake alikaa kipindi kimoja tu, hii inawaumiza sukuma gang mpaka kufa
 
Wewe kubali tu tuko awamu ya 5. 2020 tumemchagua magufuli wewe jitahidi kuendeleza msimamo wa kimagufuli ndio watu walimchagua. Ukifanikisha hilo hakika watu watakupenda sana. Mungu akubariki mama yetu.
Hivi magufuli aliwahi kushinda uchaguzi wote tangu akiwa mbunge ??
 
Mbona hili liko wazi kabisa ,halihitaji hata tochi,awamu Ni mtu na Wala so miaka Wala vipindi,so hii Ni serikali ya awamu ya sita
 
... wanagombea awamu! Ajabu kweli kweli! Mama hataki kujinasibisha na awamu ya 5; wao wanajaribu kum-drag arudi awamu ya 5! Sijajua kila upande una siri gani ila kama unavyosema to common mwananchi awamu is immaterial or better call it NONSENSE!
 
Unapotumia neno AMIRI JESHI maana yake ni kama unamtisha asitoe maoni yake
 
Polepole yupo sahihi, ishu ni kuwa alishajipaka sana matope enzi za godfather kiasi hakuna Mtanzania anayemtilia maanani sasa...
 
Polepole hataki ubunge, ... msimlazimishe!
... kama eye hataki ubunge atuachie nasisi sasa tuchukue ubunge! (kwa sauti ya Gwajiboy!😅)
 
HII NI AWAMU YA SITA, NA TUNAYE RAIS WA AWAMU YA SITA, HII SIO AWAMU ILE YA UDHAMU, UHUNI WA KUPIGA WATU RISASI, KUPOTEZA WATU, WAKO WAPI AKINA BEN SAANANE?, MAMA HATAKI KUJIHUSISHA NA UDHALIMU WA KIONGOZI ALIYEPITA, KWANI AKISEMA HII NI AWAMU YA SITA, MNAUMILIA NINI?
 
Hii aya ya mwisho imeonesha ni namna gani CCM hii nchi mejitwalia aisee. Inasikitisha sana!
 
Polepole anasema yupo anawafuatilia watu fulani. Ambao hakuwataja kwa jina ila amesha wapa warning kuwa wakivurunda atawaambia wazi wazi kuwa umevurunda. Inaonesha kuna watu wanataka waachane na ile miradi mikubwa ya awamu ya magufuli
Kwani nchi hii ni ya Magufuli.?
 
Nchi haiendeshwi kwa ilani ya chama bali Katiba na sheria, ilani inaweza kutupiliwa mbali kabisa na nchi ikaendelea. Kikwete alijenga UDOM na haikuwa kwenye ilani, Magufuli kajenga Bwawa la Stiglers na Daraja la Kigongo Busisi bila kuwepo kwenye ilani.
Mang'ula amesema ilani ya uchaguzi ilizunguzia kujenga gati bagamoyo huyu rais atuonyeshe ilani yake aliyoingia nayo kwenye uchaguzi
 
Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21 alitawala kwa awamu ngapi?
Inawezekana polepole yuko sahihi kwa maana kwamba aliyebadilika ni rais peke yake. Kwa hiyo tunaweza kusema Samia ni rais wa sita katika awamu ya tano
 
Hili tulilo nalo ni bunge la kumi na mbili.
 
Hujui chochote kuhusu katiba, katiba haina propoganda za awamu.
Katiba inasemaje..au tunaedeshwa ni mtu mmoja kwa mawazo yake..kwahiyo angesem awamu ya 10 mngekenua meno tu..njaa ya kichwani mbaya sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…