Polepole avumiliwe tu atoe maoni yake, ni haki yake kisheria, na naona itapendeza zaidi kama hoja zake zikijibiwa kwa hoja sioni sababu ya ku-refer alikotoka au alichowahi kusema.
Nasema hivyo nikiwa na maana kwamba, Polepole asijekuwa na pointi ya msingi halafu tukashindwa kuisikiliza kwasababu ya kumuhukumu kwa past.
Inajulikana wapo baadhi ya wanasiasa waliowahi kuongea pumba siku za nyuma lakini leo wakiongea tunawasikiliza, kwanini isiwe hivyo kwa Polepole?
Haki ya mtu lazima iheshimiwe bila kujali amewahi kufanya nini au kusema nini siku za nyuma, kuipigania haki yako lazima uipiganie kwa mwenzako pia unapoona kile unachokipigania wewe anadhulumiwa bila kujali yuko upande upi kiitikadi.