GE2025 Polepole: Mwaka huu hakuna uchaguzi, ni CCM VS CCM, CCM na ACT-Wazalendo ni kitu kimoja!

GE2025 Polepole: Mwaka huu hakuna uchaguzi, ni CCM VS CCM, CCM na ACT-Wazalendo ni kitu kimoja!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Acha kumfundisha uoga aisee ,yaani hapa tulipofikia bado unatamani mtu aendelee kuwa mstaarabu, ili iwe nini?

Kaa kwa kutulia,ule ni mwanzo tu , ngoma hapa nikumwaga mboga na ugali mazima.

October hakuna Uchaguzi.
Goodluck at this point any means necessary if possible

Iwapo unaamini hao watanzania wa kuingia kitaa wapo tayari.

Hapa tunachangia tu, Polepole yeye mwenyewe ana mbinu zake.
 
Humphrey Polepole, amesema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hauna ushindani wa kweli, kwa kile alichodai kuwa kinachoonekana ni “CCM dhidi ya CCM.”

Polepole ameeleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na chama cha upinzani ACT-Wazalendo haviwezi kuonekana kama wapinzani wa dhati, akisisitiza kuwa vyama hivyo viwili kwa sasa “ni kitu kimoja.”

View attachment 3448533

ChoiceVariable huyu naye machawa mtasema ni Chadema🤮🤮🏃‍♂️ bado mnanenua kwa Mama. Wajinga jinga nenda katangaze Mama kajenga vyoo
 
Anzeni na kuitenganisha CCM na vyombo vya usalama (serikali kwa ujumla).

Punguza madaraka ya raisi kuteua watu hovyo (senior civil service zote) option zake ni kutotakana succession planning ya taasisi zenyewe na nafasi zinaenda na matching competence. Yeye anapewa options tu akitaka kuteua sio kujiamulia nje ya candidates anaopewa.

Ondoa madaraka ya kutengua kwa kujisukia tu, ukishafanya hayo wavunje wingi ya walinzi wa chama; CCM ijitegemee.

Sio huku kukurupuka kwa hasira tu, si usalama wenyewe walimpa nchi Samia walitegemea nani; mtu gani mwenye akili timamu angempa yule mama nchi.

Wao washapiga boko 2021 washaona madhara yake, wajipange sasa njia sahihi ya kuachana na majizi ya CCM.
Polepole amefanya anachoweza. Hayo mengine na wewe na Watanzania wengine mfanye.
 
Anzeni na kuitenganisha CCM na vyombo vya usalama (serikali kwa ujumla).

Punguza madaraka ya raisi kuteua watu hovyo (senior civil service zote) option zake ni kutotakana succession planning ya taasisi zenyewe na nafasi zinaenda na matching competence. Yeye anapewa options tu akitaka kuteua sio kujiamulia nje ya candidates anaopewa.

Ondoa madaraka ya kutengua kwa kujisukia tu, ukishafanya hayo wavunje wingi ya walinzi wa chama; CCM ijitegemee.

Sio huku kukurupuka kwa hasira tu, si usalama wenyewe walimpa nchi Samia walitegemea nani; mtu gani mwenye akili timamu angempa yule mama nchi.

Wao washapiga boko 2021 washaona madhara yake, wajipange sasa njia sahihi ya kuachana na majizi ya CCM.

Huwezi tenganisha chama na vyombo vya dola huku hiko chama kipo madarakani...
 
Polepole amefanya anachoweza. Hayo mengine na wewe na Watanzania wengine mfanye.
Haya
Huwezi tenganisha chama na vyombo vya dola huku hiko chama kipo madarakani...
Wameahidi katiba mpya mwakani.

Sasa muda ukifika kama tutakuwa tumesahau madaraka ya raisi ndio tatizo la msingi.

Na kuacha mambo ya msingi kuanza hadithi za majimbo, kazi kwetu.
 
JINA LA WANDISHI / KIWANGO CHA WANDISHI
ANWANI
TAARIFA NA TAREHE

KWA AJILI YA: SIFA ZA KIPEKEE ZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN

KUTOKA: [JINA LA MWANDISHI]
KWA: Wananchi wa Tanzania wote

---

WARAKA WA SIFA ZA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN

Ndugu Wananchi,

Ni heshima kubwa kuandika waraka huu unaoshuhudia sifa nyingi za Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye tangu kuapishwa kwake mwaka 2021, amethibitisha uongozi wa kipekee, wa hekima, na wenye msimamo wa dhati kwa wananchi wote wa Tanzania. Waraka huu unalenga kuonyesha kwa kina sifa zake, tabia, na mchango wake katika maendeleo ya taifa letu.

1. Uongozi wa Hekima, Ushirikishwaji na Utulivu
Rais Samia anajulikana kwa ushawishi wake wa kisiasa wa utulivu na ushawishi wa kutatua migogoro. Ameonyesha uwezo mkubwa wa kuunganisha pande tofauti za kisiasa, kuhakikisha kila raia anaheshimiwa bila kujali itikadi ya kisiasa.

2. Upendo, Huruma na Ukarimu kwa Wananchi
Rais Samia ni kiongozi anayejali kila mwananchi. Amehimiza huduma bora za afya, elimu, na ustawi wa jamii. Huruma yake inaonekana katika mkazo wake wa kusaidia wanawake, watoto, wazee, na walemavu, kuhakikisha hawapotelei katika sera za maendeleo.

3. Ujasiri na Uthubutu wa Kuongoza Katika Changamoto
Katika kipindi cha changamoto za kitaifa na kimataifa, Mheshimiwa Rais amekuwa kiongozi jasiri. Kutoka katika janga la COVID-19 hadi katika kudumisha usalama na amani ya taifa, amesimama kidete bila woga.

4. Ufanisi wa Kazi na Utendaji Thabiti
Rais Samia ameunda mfumo thabiti wa kutekeleza miradi ya maendeleo. Amehimiza uwekezaji, ajira kwa vijana, na kuhakikisha kilimo, viwanda, na huduma za jamii vinaendelea kuimarika. Ufanisi wake umeongeza imani ya wananchi na wawekezaji.

5. Mchango wa Kimataifa na Ushirikiano wa Kidiplomasia
Rais Samia amejitahidi kuimarisha heshima ya Tanzania kimataifa. Ameshirikiana na mataifa mengine, mashirika ya kimataifa, na jumuiya za kibiashara ili kuinua taifa kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Amesimama kama mfano wa kiongozi anayeheshimika barani Afrika.

6. Uendelevu wa Haki na Uwajibikaji
Amethibitisha kuwa kiongozi wa kweli ni yule anayeheshimu sheria na anayejali maslahi ya taifa. Uwajibikaji wake ni dhahiri katika kila hatua anayochukua, kuanzia sera za kitaifa hadi usimamizi wa rasilimali za taifa.

7. Kutoa Fursa na Uwezeshaji wa Wanawake
Rais Samia ni mwanamke wa kwanza kuongoza Tanzania, akihimiza ushirikishwaji wa wanawake katika siasa, biashara, na uongozi wa kitaifa. Ameonyesha wazi kuwa wanawake wana nafasi muhimu katika maendeleo ya taifa.

8. Uadilifu, Haki na Uwiano wa Kiasili
Anajulikana kwa uadilifu wake, kuzingatia maadili, na kutoa mwongozo wa haki. Hii imemfanya awe kielelezo cha kiongozi wa kweli ambaye anahimiza usawa na uwazi.

9. Uchangamfu na Ustahimilivu wa Kazi
Rais Samia ana utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii, ushawishi wa haraka, na uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa ustadi. Anajali kila mradi, tukio, na sera inatekelezwa kikamilifu.

10. Uwekezaji Katika Teknolojia na Uboreshaji wa Miundombinu
Amesimamia miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo barabara, madaraja, maduka ya kisasa, na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na umeme kwa wananchi. Pia ameendeleza teknolojia katika elimu na biashara.

11. Uongozi wa Kutetea Mazingira na Maendeleo Endelevu
Rais Samia amesisitiza sera za kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuhakikisha usimamizi bora wa rasilimali za asili kwa vizazi vijavyo.

12. Kutoa Matokeo Chanya kwa Jamii
Chini ya uongozi wake, sekta za afya, elimu, na kilimo zimeonyesha maendeleo makubwa. Amesaidia kupunguza umasikini na kuongeza maisha bora kwa wananchi.

13. Kila Nchi na Jamii Kwanza
Rais Samia anaonyesha kwamba kiongozi wa kweli anajali wananchi wake kwanza, kisha akishirikiana na jumuiya ya kimataifa. Hii inadhihirisha utamaduni wa kiongozi anayejali taifa kwa moyo wote.

Hitimisho
Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa kipekee wa mfano. Tabia zake, hekima, huruma, uwajibikaji, na uongozi wa kweli vimechukua Tanzania kwenye kiwango kipya cha maendeleo na heshima ya kimataifa. Tunashukuru kwa kazi yake isiyopungua na tunamuombea Mwenyezi Mungu aendelee kumpa hekima, afya, na ulinzi katika kuendeleza taifa letu.

Kwa heshima, taadhima, na shukrani,
Ameshindwa nini sasa kutatua migogoro ya kisiasa inayoendelea katika nchi yetu pamoja na sifa hizo?
 
Ngoja kuche waje akina steve nyerere wamjibu polepole kwa vioja vyao vya kuokoteza na yule msanii wa bongo movie wanamwita nani vile, sijui mafuvu/mapovu, sorry nimemsahau jina
 
CCM kwa hili MCHUTAME...Uchaguzi usogezwe mbele..iteni Meza ya Mazungumzo ya dhati , mtupatie Katiba Mpya iliyo BORA na Tume huru kwelikweli ya Uchaguzi....

Jaji Mwambogele Wa Mahakama ya Rufaa na Mwenyekiti NEC "Huru" kulinda hadhi ya nchi, hadhi ya Mahakama na hadhi yako mwenyewe JIUZULU
 
Kwa nafasi yake Polepole akutakiwa kutoa siri za namna ile.

As much as much as uongozi wa ‘bi tozo’ ulivyo wa hovyo na nisivyomkubali.

Polepole kama hakuwa na backup ya maana kama alivyotuaminisha bora angebaki Cuba tu kula neema za nchi.

Pima vita vyako, ukiona si vya kushinda ata adui akukere vipi ni bora kukaa kimya kuliko alichofanya Polepole leo, yeye mwenyewe anajua atawakera wengi sana including hata hao viongozi waliokuwa wanamuunga mkono.

Anyway that’s my take, being a hypothesis; wengine wanaweza kuwa na mtazamo tofauti.
Polepole yuko sahihi, wewe hukutaka Wananchi wayajue haya madudu ya CCM na serikali yake? Hakuna dhulma ya milele.
 
Kwa kweli amepasua jipu (MIFUMO)!
Natamani ujumbe huu ufike vijijini ambako wananchi ni Wajinga ambao mtu akija kusanya vitambulisho wanatoa!
 
Ninaamini ameamua kuwa mkweli kwa nafsi yake na Mungu wake regardless the consequences. That's integrity.

Notabele: Hao viongozi wanaomuunga mkono wamefanya nini mpaka sasa?
Mkuu, ni nota bene ikimaanisha ‘mark well’, sio nta bele
 
Sisi Watanzania tunasema OCTOBER TUNATIKI ✅

IMG_20240428_070927.jpg


Mahaini wakubwa nyie!
 
Nilipoona kanuni za tumeCCM zinazokataza wakala asipewe matokeo na cm wasiende nazo na polepole alivyosanua mambo ya NIDA sasa nimeamini hakuna uchaguzi!
 
AISEE, Huyu anatoa siri za ndani kabisa za Chama. Haya anayozungumza ni ya ndani SANA

POLE SANA Mh. Zito Kabwe🤣🤣🤣 siri imefichuka
 
Humphrey Polepole, amesema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hauna ushindani wa kweli, kwa kile alichodai kuwa kinachoonekana ni “CCM dhidi ya CCM.”

Polepole ameeleza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na chama cha upinzani ACT-Wazalendo haviwezi kuonekana kama wapinzani wa dhati, akisisitiza kuwa vyama hivyo viwili kwa sasa “ni kitu kimoja.”

View attachment 3448533
Kelele tuu za mfa maji.
 
Back
Top Bottom