Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba


Wakati Uliokubalika Ni Sasa Hivi Ccm Inaendelea Kubomoka

SARUJI Na Nondo Zimeshindwa Kuzuia Nyufa!!!
 
Kwenye vitabu vya dini ,vinasema Luqman alitoa usia kwa mwanawe,kuwa awe anachunga ulimi wake,kwa maana ulimi unaumba/unaojenga na ulimi unabomoa.Ni maneno yenye busara na hekma ukiyazingatia katika maisha.
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
Na kweli mambo ya kihayawani wanajuana na ukijani kibichi . Walanguzi wa nchi yetu mnachosha
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
We boya kweli, Lisu yupo mamtoni anakula bata we mpori pori upo unaharisha hapa.
Mambo mengine muwe mnatumia akili kidogo. Huyo Lisu ni nani? Na anamsaada gani nchi hii? Km ni mzalendo kweli kinachomfanya ang'ang'anie kwa wazungu ni kipi? Kwanini asirudi apambane hapahapa. Maana aliodai wanataka kumuua hawapo!
 
Hata Pharaoh aliwatesa wana wa Israel, Musa akaja kuwaokoa. Muda siku zote unaponya hakuna aliye mbele ya muda. Je, yupo aliye mbele ya muda ?Relax , Be Humble !!
 
Yuko sahihi ila anaelewa kua mawaziri hawawezi kufanya ivo.

Hali aliyokua nayo kipindi cha mwendazake ndiyo hiyo hiyo wanayo mawaziri sasa hivi. Kama yeye alishindwa kukemea unyama wa viongozi kwa wakati ule asitegemee kuna wanaoweza sasa.

Lakini ni afadhari leo yupo huyu aliejitokeza na kukemea ambae ni ccm mwenzao kuliko kipindi kile cha mwendazake hakuepo mwanaccm hata wa kusema su.

Kama sio propaganda za kisiasa basi nampongeza ila kama ni janja janja ya chama chake ni bora akaacha tu.
 
View attachment 2100413
"Wapo watu wanakula urefu wa Kamba na wanavimbiwa, hivi hawa watu wana uhalali wa kutuambia sisi tuishi maisha ya uadilifu? na mimi nitakuwa nauliza na wewe unakula kwa urefu wa kamba? kama ndio basi usiongee na mimi". Polepole

"Mimi nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba kwamba kuna wenzetu wanakula kwa urefu wa kamba na kauli hii haikubaliki, mimi nilidhani watu watatoka, lakini wapi ni kwa sababu ni wanafiki" Polepole

Pia, soma: Thread 'Rais Samia: Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, lakini mbona mnakula sana mnavimbiwa? Si kweli kama hampati kwenye maeneo yenu. Jipimieni...' Rais Samia: Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, lakini mbona mnakula sana mnavimbiwa? Si kweli kama hampati kwenye maeneo yenu. Jipimieni...
Comredi Polepole endelea kupambana na hao wahuni mpaka kieleweke.

Ila hapo kwa mawaziri kukemea kulaani kauli ya bosi wao umechemka, Rais wa Tz huwa hakosei.
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
Hata ikipita miaka 10,kuna umuhimu wa tume huru kuundwa, ili kuchunguza na kuwataja hadharani wale wote waliohusika kwenye matukio ya mauaji/kupotezwa watu wasio na hatia, kupigwa risasi TUNDU LISSU chini ya utawala wa MAGUFULI, na report hiyo isiache mashaka yoyote, hata kama wamekufa watajwe tujue...
 
Polepole kwa sasa(hizi siku baada ya kunyang'anywa mkate wa marehemu asiendelee kuubugia) anaweza kuwa anaongea vitu vya maana sana tu.Lakini alishajiondolea kuaminika kwa umma.Aangalie na ajifunze upya alipokosea.
 
Back
Top Bottom