Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

Kinachoendelea kwa Magufuli sio kwamba alikuwa kiongozi mbaya au dikteta ni chuki na visasi kwa kuwatumbua vyeti feki, kupinga ufisadi na rushwa, ukwepaji kodi, kuzuia uuzaji madawa ya kulevya, waliojenga kiholela mabarabarani ,wadhulumaji ndio wanaoendesha chuki kwa magufuli kwa kimvuli cha lisu kupigwa risasi, akwilini, Ben saanane kupotea sijui democrasia unafiki mtupu hawana uchungu na hizo haki za binadamu ni maslahi yao binafsi
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
Lissu kibaraka wa mabeberu aliye tutishia kuwa tutashitakiwa na wazungu kwa kuwadhibiti wasituibie
 
Pole pole kamba yako kwasasa imekuwa fupi mno malisho yameanza kuisha ndio maana tunaanza kusikia kelele kipindi kamba yako ilipokuwa ndefu kipindi kile Cha JPM ulibaki kujigamba tu na kuisifia V8 kwahiyo tulia na wenzako waongezewe urefu wa kamba wale
 
Magufuli hawezi kuongea huo ujinga wa kula kwa urefu wa kamba! Waacheni wale kwa urefu wa kambana kufanya birthday!
Nchi ina amani mi naona ndio jambo kuu, hakuna watu kutekwa, kuibiwa fedha zao za kigeni kwenye maduka live live, makesi ya kubambika kama zimepungua sana, watu kuishi kwa khofu jamaa kesho ataamkaje, watu kuvunjiwa majumba yao, kupotezwa na kudhalilishwa kwa kupimwa vinasaba na kunyimwa haki za uraia, wenye mashamba yao kunyanganywa kwa nguvu na dola, watu wasiojulikana kutesa watu, kuibia watu kuuliwa bila majibu alimradi haya mambo yameondoka nadhani tuna amaani,
 
Sidhani kama hata form two failure umefika, its either std 7 failure au mchunga mbizi wa waziri. Nonsense
 
CCM mkirudia kosa mlilotufanyia 2015 na nyie tutawszika chato naona kwenye lichama lenu Kuna mabaki ya yule nyang'au wenu mliemwokota huko chato,mkamleta mjini Lumumba.
 
Lkn hii ni “free Country“ na ana haki ya kutoa maoni yake kama Mbunge, kosa lake ni lipi ? Mbunge hapaswi kukosoa au kutoa maoni yake tena ?

Polepole ni Mbunge, kaona Serikali haifanyi sawa, anaikosoa, kosa liko wapi ?
Spika kakosoa tu wakamvamia nchi nzima sembuse huyo mbunge !!?
 
Huyu nae vip, mbona kipindi cha mwendazake alikua kimya, alivyokua akiwaambia watu kua, wataishi Kama mashetani, kila atarudi kijijini na kuondoka dar, pia aliwaambia wana kagera kua Mimi sikuleta tetemeko, kaeni na Mav.I yenu . na maneno mengi mengi machafu , kwa alikua wapi kipindi hicho kukemea , mwambieni akae kwa kutilia
 
Alishapoteza ushujaa muda mrefu, hapo alipo analazimisha ushujaa uchwara. Unyama mwingi ulifanyika kwenye utawala wa Magufuli na alifurahia kwani alikuwa kwenye mlo, sasa hivi hayupo kwenye ulaji ndio anatafuta kick ili arudi kwenye mlo tena.
Tulimwambia hakusikia na sasa hayupo!!Uzi wa Tumiaakili huo kausome!! Pole pole anasema kama alivyoelekezwa kusema!! pole pole alikaa kimya hakuwa na la kufanya angefanya nini??ili na yeye afe??sio kila mtu Anaweza kufia wengine ila kusemea wengine!!!
 
Kuna kitu kimoja mkuu hujaelewa hapo hapingi kwasababu ya uwana harakati ila alicho nacho ni chuki na kumkomoa Kwa kupinga kila kitu anachosema ata kama ni cha kweli kwasababu tu alikuwepo awamu ya Tano.

NB. Punguza maneno makali tujadili na kutoa maoni yetu bila kuvunjiana heshima.
 
Polepole akubali tu mambo yamebadilika baada ya mungu wake kufariki aache masononeko atajiumiza bure apate maradhi ya kujitakia.
 
CHADEMA ni chama tawala?
Shame on you.
 

kashakata kamba anaenda kula mahindi kwenye mashamba ya watu.
Mbuzi huwezi tu ukamwacha umemfunga tu kila siku ale kwenye urefu wa kamba yake siku nyingine achelewi kukata kamba na kwenda kuvamia mashamba ya watu .
Mbuzi hata ukimfunga kamba lazima umchunge asije kata kamba na kuingia kwenye mashamba ya watu , huyu maza nazani hajawai kufuga mbuzi wa kufungwa kamba anajiongelesha tu kizembezembe
 
Polepole awe mpole kamba yake ilishakatika awaachie wengine nao wale
Wakati wa Magufuli hamkuwa mnasema haya kwa kina Nnape February na washirika wao although wao wamerudi kula na hawataki kuwaachia wengine, hamseni kabisa yaani vile ni unafiki, roho mbaya and others same like this...
 
kama uungi mkono mtu mnafiki mbona unamuunga mkono Tundu lissu aliwahi kumshambulia Lowassa kuwa ni fisadi na huyo huyo akampokea kwenye chama chao na pia akamfanyia mpaka kampeni uoni kuwa unafanya double standard?
 
Shida sio kumpokea Lowassa shida ni unafiki waliouonesha kwa kumpokea mtu ambaye wao wenyewe walimtuhumu kuwa ni fisadi na wanaushahidi na ufisadi wake nawakaenda mbali zaidi mpaka wakamuweka kwenye list of shames inakuaje huyo huyo mnampokea na anakuwa mgombea wenu wa uraisi? Hoja kuu Mnamwita PolePole ni mnafiki mbona karibia wanasiasa wote ni wanafiki ikiwamo hao wa Chadema pamoja na unafiki wa viongozi wa Chadema waliwahi kuonesha na wengine pia wanaonesha recently lakini mnawasiliza hoja zao kwanini kwa PolePole iwe mnafanya personal attack badala ya kujadili hoja zake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…