benignusmulisa
Senior Member
- Feb 4, 2014
- 150
- 167
Mwenyezi Mungu atangulie. Amani ya Bwana iwe nanyi, na rehema za Allah ziwe juu yenu nyote.
Katika mahojiano ya moja kwa moja usiku wa leo, aliyekuwa mbunge na mwanasiasa machachari, Mhe. Humphrey Polepole, alipokea swali kutoka kwa mmoja wa Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora). Swali hilo lilikuwa la moja kwa moja na lenye kugusa hisia:
"Je, unajua kuwa Mzee Warioba yupo chini ya kifungo cha ndani (under house arrest)?"
Katika kujibu, Polepole alisema hana mawasiliano ya moja kwa moja na Mzee Warioba, lakini ana rafiki wa karibu wa Warioba ambaye huwa anawasiliana naye. Kwa mujibu wa Polepole, mara ya mwisho alielezwa kwamba Mzee Warioba alikuwa salama, na alituma salamu kwake kupitia huyo rafiki.
Kauli hii, badala ya kuondoa wasiwasi, imezidi kuzua taharuki miongoni mwetu. Swali linabaki:
My take
JE, NI KWELI MZEE WARIOBA YUPO CHINI YA KIFUNGO CHA NDANI?
Historia Fupi ya Mzee Warioba
Jaji Joseph Sinde Warioba ni Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1985–1990), na baadaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2012. Ametambulika kwa uadilifu, uzalendo, na uwazi katika kuzungumzia masuala ya haki, utawala bora na Katiba ya wananchi.
1. Kutokuwepo hadharani kwa muda mrefu – Kama mdau nimegundua kimya cha muda mrefu kutoka kwa Mzee Warioba, tofauti na desturi yake ya kutoa maoni kwenye masuala ya kitaifa.
2. Kauli ya Polepole – Badala ya kusema kwa uhakika kuwa Warioba yuko huru, alijibu kwa njia ya kusita na kuleta mtu wa kati kama chanzo cha taarifa. Hili linazua maswali.
3. Ukimya wa vyombo vya habari. Hakuna taarifa rasmi kutoka serikalini wala vyombo vya habari kuhusu hali ya Mzee Warioba, jambo ambalo linazua hisia kuwa kuna jambo linafichwa.
4.Kauli ya Kikwete kuhusu viongozi wastaafu wanaopenda kuita press pindi wanapotaka kukosoa jambo la kitaifa. Ile kauli yake ilikuwa ya kufikilisha.
Wito kwa Wananchi na Majirani
Kwa kuwa Mzee Warioba anaishi maeneo ya Dar es Salaam (inayosemekana ni Mikocheni au Kunduchi), tunatoa wito kwa majirani, viongozi wa mtaa, na wale wenye taarifa za uhakika kutupa mrejesho kuhusu hali ya mzee huyu. Je, anaonekana? Ana wageni? Anazunguka?
Ikiwa ni kweli kuna vizuizi dhidi yake, basi Watanzania wana haki ya kujua sababu, kwani huyu ni hazina ya taifa, kiongozi wa kiadilifu ambaye alihudumu kwa bidii, si kwa maslahi binafsi bali kwa mustakabali wa taifa.
Wadau, je huu ni uvumi au kuna ukweli ndani yake? Tunahitaji majibu.