Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Komredi Polepole yuko mubashara Channel ten akizungumzia maendeleo ya kampeni za CCM.

Kadhalika Polepole ametolea ufafanuzi baadhi ya mambo yaliyopotoshwa na wapinzani hasa Tundu Lisu ikiwemo ujenzi wa SGR na uwanja wa ndege wa Chato.

Karibu.

=======

POLEPOLE: Wenzetu wa Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi. Lakini uzuri Watanzania wanajua uongo na leo nitawapeni ushahidi wa mambo ya uongo watu hawa wamesema.

Ukija kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege, kiwanja cha ndege hatujajenga Chato peke yake. Tunajenga Singida, Mpanda. Na kwanini tumejenga Mpanda? Juzi anasema uwanja wa ndege wa Mpanda umejaa majani, hivi kweli?

Mimi sipendi kuzungumza mambo ya mtu binafsi, nafahamu mwaka 2017 huyu bwana alipata matatizo, matatizo wanapata watu wengi lakini nna shaka somewhere, somehow pahala fulani hivi iko shida kwenye memory.

Uwanja wa ndege wa Mpanda haukujengwa kwa sababu ya Mizengo Pinda, uwanja wa ndege wa Mpanda ambao unafanya kazi mpaka leo hii asubuhi, ndege inatua pale ya bombadier, abiria wengi wanaotumia uwanja wa ndege wa Mpanda sasa hivi ni watalii. Wanakwenda Katavi National Park yenye wanyama mbalimbali.

Ukiangalia flight manifest ya abiria wanaokwenda Mpanda, wengi ni raia wa kigeni.
 
Vipi Kuhusu mifuko ya jamii na Mafao?

Pole pole amejibu Kuhusu FAO la kujitoa na kuchelewa Malipo?

Na ardhi eka 25000? Amejibu huyo


Je kurudishia watu Pesa zao za vitambulisho?
Kuwa mpole utajibiwa bwashee!
 
Kwa jinsi hali ilivyo ni kama wapinzani walikuwa hawajafungiwa miaka 5 kufanya siasa..... Watu wako very inspired.
Nadhani hata CCM hawaamini kinachoendelea....

Hili la Polepole kujitokeza na kujibu linazidi kuzidisha moto wa kifuu....


The battle still continues!!!!!
 
Back
Top Bottom