Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Mimi nilifikiri atapangua hoja za wizi wa ardhi Karagwe na utoaji ajira wa kupendelea mtoto wa Dada na Dotto James
 
Polepole tulishamzoea kwamba ni mnafiki wa aina ya wale watu anayeweza hata kukana jina lake mwenyewe! Polepole yule wa Tume ya Jaji Warioba sio huyu anayeongea sasa!

Kamwe hawawezi kuiokoa CCM kwa kucheza mziki anaopiga Lissu! Hayo mambo ya Chato, SGR na vingine kila mfuatiliaji wa mambo hapa nchini anayajua na anajua dosari zake ila tu watu wapo kimya sababu wamenyimwsa uhuru wa kuongea!

Lissu sasa amekuwa sauti ya wengi walio kimya ndio kisa cha kujaza nyomi katika mikutano yake sababu anaongea masuala yanyogusa wengi! Polepole na CCM yake waje na sera za matumaini mapya kwa wanchi na sio kukariri ilani za vyama vingine!

Wakulima walishapigika, wanalima lakini soko la mazao hakuna! Vijana wanasoma huku wazazi wakijifilisi kwa kuuza ng'ombe na viwanja, lakini wakimaliza vyuo ajira hakuna!

Watumishi waliambiwa wachape kazi kufa na kupona kupitia slogani ya Hapa kazi tu, wamejikamua kuchapa kazi, lakini mishahara mipya na madaraja hakuna! Wavuvi wana mazingira magumu sana, wanashindwa kufikia bei ya vibali vya uvuvi, wameishia kukamatwa na kuchomewa nyavu badala ya kuwawezesha!

Wastaafu wanazungushwa mafao yao ambayo ni michango yao waliyo changia katika mifuko bila kuzungusha wa kuleta usumbufu wowote, Lakini leo huku mishahara yao ikiwa ilishasitishwa, bado wamekuwa watu wa nenda rudi, nenda rudi huku maisha yakiwa ni magumu sana!

Wanufaika wa Bodi ya mikopo, wanalia na marejesho ya 15% wanataka unafuu wa marejesho hayo! Waliobomolewa nyumba zao bila fidia, wengine mpaka leo hawajanunua hata viwanja, wote hawa wanaungua na ugumu wa maisha, wanataka sera zitakazowapa unafuu! Hivyo Polepole kama ana hoja ajibu kwanza haya!
 
Hakuna wa Kumjibu Lissu CCM kwa sasa.. Vinginevyo ni Kujichafua na Kujivua Nguo. CCM watulie wasijibu Hoja za Lissu maana Zinawaumiza sana Watanzania anavyozidadavua. Hotuba za Lissu ni Kitu Black and White.. Hakuna Chenga ati... Nyeupe ni Nyeupe na Nyeusi ni Nyeusi ...
Uzuri wewe si muamuzi wa mwisho juu ya urais
 
Namsikiliza hapa, jamaa anatupa nondo kali amepangua hoja zake kwa ushahidi na kisomi sana. Sema naye kaamua kumtukana live Lissu😂. Anamuita jambazi, mnafiki, tapeli, mjinga na mtu asiyekuwa na kumbukumbu vizuri. Niliona ni kama kamkosea heshima Ila kwa sababu alizotoa, nimekubali.
 
Polepole tulishamzoea kwamba ni mnafiki wa aina ya wale watu anayeweza hata kukana jina lake mwenyewe! Polepole yule wa Tume ya Jaji warioba sio huyu anayeongea sasa! Kamwe hawawezi kuiokoa CCM kwa kucheza mziki anaopiga Lissu! Hayo mambo ya Chato , SGR na vingine kila mfuatiliaji wa mambo hapa nchini anayajua na anajua dosari zake, ila tu watu wapo kimya sababu wamenyimwsa uhuru wa kuongea!...
Mkuu uko sahihi Polepole wakati wa kampeni 2015 alikuwepo kwenye kampeni team ya CCM na alikuwa mstari wa mbele kumkuwadia jiwe kuwa lazima atatuleta katiba mpya. Polepole huyu huyu aliibika na kusema katiba siyo kipaumbele cha CCM yeye na Palamaganda Hawa watu hawaaminiki
 
Wenzetu wa upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi. Lakini uzuri watanzania wanajua uongo na leo nitawapeni ushahidi wa mambo ya uongo watu hawa wamesema...
Tunaongelea uwanja wa ndege wa kijiji cha CHATO, wewe unazungumzia viwanja vingine, What kind of defense is that? Ongelea uwanja wa CHATO. Tunajua viwanja vingine kwa nini vimejengwa. Unamtukana mwenzio, je wewe tukikwambia una sura ya kizee....Utalia wewe?
 
Lissu aje afanye mdahalo na mtu wa level yake Humphrey Polepole.
 
Hakika wapinzani ni waongo sana tena saaaana,yaani waliahidi vitu 2015 mpk leo hawajavitekeleza'.

Screenshot_2020-09-24-19-55-15-1.jpg
 
Wakuuu Polepole yuko na tvccm anafoka foka, Mwaka huuu atajua ajui sisi watanzania wote tumeamua kumpiga chini magufuli hivyo hana chake hapa sisi tumeamua ni lisu tu, wao wamejimilikisha nchi sasa wameshangaaa lisu anavyowapepeta watajua hawajui...
2020-2025
NI JPM TENA.
 
Tunaongelea uwanja wa ndege wa kijiji cha CHATO, wewe unazungumzia viwanja vingine, What kind of defense is that? Ongelea uwanja wa CHATO. Tunajua viwanja vingine kwa nini vimejengwa. Unamtukana mwenzio, je wewe tukikwambia una sura ya kizee....Utalia wewe?
Na Tundu Lissu wala asipoteze muda wa kumjibu huyu mchumia tumbo lake maana tumeshamjua ni kilaza fulani ambae haiwezi kusimamia Jambo lake mwenyewe.
 
Polepole alisema iwapo uchaguzi utakua huru na haki basi CCM kijiandae kukabizi dola sasa Leo anakuja na ngonjera gani tena
Tanzania ya Leo sio ile ya kipindi kile anazungumza hivyo..!
 
Back
Top Bottom