Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Uchaguzi 2020 Polepole: Upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, adai Lissu ana tatizo la 'memory'

Komredi Polepole yuko mubashara Channel ten akizungumzia maendeleo ya kampeni za CCM.

Kadhalika Polepole ametolea ufafanuzi baadhi ya mambo yaliyopotoshwa na wapinzani hasa Tundu Lisu ikiwemo ujenzi wa SGR na uwanja wa ndege wa Chato.

Karibu.

Up dates;
Kwa hiyo Lissu aliudanganya umma,uwanja wa ndege wa Chato haukujengwa?
 
Wenzetu wa upinzani wamekuwa mstari wa mbele kutumia uongo kama nyenzo ya kampeni, uongo mkubwa, upotoshaji wa makusudi. Lakini uzuri watanzania wanajua uongo na leo nitawapeni ushahidi wa mambo ya uongo watu hawa wamesema.

Ukija kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege, kiwanja cha ndege hatujajenga Chato peke yake. Tunajenga Singida, Mpanda. Na kwanini tumejenga Mpanda? Juzi anasema uwanja wa ndege wa Mpanda umejaa majani, hivi kweli?

Mimi sipendi kuzungumza mambo ya mtu binafsi, nafahamu mwaka 2017 huyu bwana alipata matatizo, amatatizo wanapata watu wengi lakini nna shaka somewhere, somehow pahala fulani hivi iko shida kwenye memory.

Uwanja wa ndege wa Mpanda haukujengwa kwa sababu ya Mizengo Pinda, uwanja wa ndege wa Mpanda ambao unafanya kazi mpaka leo hii asubuhi, ndege inatua pale ya bombadier, abiria wengi wanaotumia uwanja wa ndege wa Mpanda sasa hivi ni watalii.
 
Komredi Polepole yuko mubashara Channel ten akizungumzia maendeleo ya kampeni za CCM.

Kadhalika Polepole ametolea ufafanuzi baadhi ya mambo yaliyopotoshwa na wapinzani hasa Tundu Lisu ikiwemo ujenzi wa SGR na uwanja wa ndege wa Chato.

Karibu.

Up dates;
Naomba ajibu natoka uchomaji nyavu halali pia nahawatu wa vyeti feki ambao wametuzalishia watumishi wengi
Waalim
Madoctor
Wanajeshi
Nashangaa haya hayasemi hata hoja anazojibu zimemshinda
 
Lissu atawatesa sana mwaka huu. Kwanza ji baba lenyewe ndilo linatakiwa kujibu sio linafanya hovyo halafu linawatuma akina polopolo wakajibu.
 
With due respect Lissu ni presidential candidate.

Hivyo haya anayoyasema yanatakiwa yasemwe na Mh Rais JPM.

Huyu Polepole inabidi aende polepole kama jina lake...in short atulie
 
Tulia bwana Polepole dawa iwaingie, kama Lissu ni mrongo basi wananchi wataamua wenyewe. Msiwe na hofu watanzania wa leo wako more informed kuliko nyie Lumumba mnavyofikiria.

Hasira hizi za watanzania ndiyo kielelezo cha kuwaambia namna mlivyoliongoza taifa lao kwa miaka mitano bila kufuata sheria na katiba za nchi hasa hasa ukandamizaji wa haki za binadamu na kuminya uhuru wa kujieleza. Hili nalo utasema ni Urongo?
 
Back
Top Bottom