Watanzania tuamke kwani hiyo ndio CCM, genge linalotaka kubaki madarakani kwa njia zozote zile.
Kuteka, kutesa, kupoteza na sasa imenuia kuzima sauti zetu Watanzania.
Huwezi kuamini, lakini hiyo hapo juu ndiyo taswira halisi ya CCM, CCM ni ile ile
...CCM ya juzi , CCM ya jana, CCM ya leo na CCM ya wakati ujao kama tutairuhusu.
Unaweza kubisha, lakini ukweli ndio huo kwamba CCM ni genge la wale wale
...CCM ya Mwinyi, CCM ya Mkapa, CCM ya Kikwete na sasa CCM ya Magufuli.
Hata CCM yenyewe inataka ionekane ni ile ile na inatamba ikidai ni ile ile,
kwa matendo inathibitisha ni ile ile na inakiri kwa majigambo kwamba ni ile ile.
Ndugu zangu Watanzania, la kuvunda halina ubani na CCM sasa basi
...CCM imezeeka, CCM imechakaa, CCM inanuka na sasa umefika muda muafaka kwa CCM kufa na kuzikwa.
Tufanye kweli mwezi October, tuondokane na utawala wa kibabe usio na busara wala hekima,
utawala usiofuata sheria na utawala wa dhulma, rushwa na ukatili.