GE2025 Polepole: Wewe unayenihoji mie sikusema wakati wa awamu ya 5, wewe ulisema awamu ipi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Balozi Humphrey Polepole awacharukia wanaohoji kwanini anayoyasema sasa ikiwemo masuala ya utekaji hakuyasema awamu ya tano, Je wao wamewahi kusema kwenye awamu ipi?

Ametolea mifano kadhaa ambayo chama cha mapinduzi kipindi cha John Magufuli walikemea utekaji na mauwaji ikiwemo yaliyotokea Kibiti mkoa wa Pwani.
 
😂😂😂😂😂
Polepole kiungo nshambuliaji moto sana akitokea sub
 
Balozi Humphrey Polepole awacharukia wanaohoji kwanini anayoyasema sasa ikiwemo masuala ya utekaji hakuyasema awamu ya tano, Je wao wamewahi kusema kwenye awamu ipi?

Ametolea mifano kadhaa ambayo chama cha mapinduzi kipindi cha John Magufuli walikemea utekaji na mauwaji ikiwemo yaliyotokea Kibiti mkoa wa Pwani.
Mwamba ni Lissu tu aliyasema wakati wa Mwinyi, Mkapa, JK na Jpm pia.
 
Hii nchi I need a break ... Mie nashukia hapa, acha nifurahie uwepo wangu Dunia. Uyo polepole na wanaccm wote ni wasaka tonge na watetezi wa matumbo Yao.

Naachia line nikiwa huku Malawi nchini Madagascar.
 
Mkuu unashuka mapema mnoooo, kaa kidogo tusogee sogee
Mkuu uvumilivu Huwa na kikomo. Kwangu kuwavumilia na kusympathise kina polepole, mpina, January na nauye ni kujikosea wewe mwenyewe.

Hawa wamekuwepo kwenye awamu zilizopita, walifumbia macho mauvu na huku wakiendelea kula Kodi zetu.

Oyaaaaa ujinga wa kuwatetea na kiwaonea huruma maccm ni kujikosea heshima Mkuu
 
Balozi Humphrey Polepole awacharukia wanaohoji kwanini anayoyasema sasa ikiwemo masuala ya utekaji hakuyasema awamu ya tano, Je wao wamewahi kusema kwenye awamu ipi?

Ametolea mifano kadhaa ambayo chama cha mapinduzi kipindi cha John Magufuli walikemea utekaji na mauwaji ikiwemo yaliyotokea Kibiti mkoa wa Pwani.
Yaliyotokea kibiti?!!!!🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Dah, ama kweli binadamu. Anyways, acha tuishi miaka yetu 60-80 tujiondokee
 
Yes ndiyo maana anawahoji wao walikuwa wapi?
Yeye angesema wanaccm wenzake ni yupi aliyehoji. Halafu mauji ya mkuranga yalifanywa siri na serekali, kiasi kwamba hata wabunge wa upinzani walipotaka yajadiliwe bungeni, spika aliagizwa azuie huo mjadala.
 
Mwamba ni Lissu tu aliyasema wakati wa Mwinyi, Mkapa, JK na Jpm pia.
Tabia hii ya kutegemea mtu mmoja tu azungumze au kuchukua hatua inashangaza sana. Katika harakati za kweli za mabadiliko, kusema pekee hakutoshi, kunahitajika zaidi ya maneno. Mfumo mbovu huondolewa na mfumo mbadala, si kwa kauli za mtu mmoja hata awe mashuhuri kiasi gani. Hizi hadithi za kila mara za kumtazama mtu mmoja kama mkombozi hazitatufikisha popote. Tundu Lissu si Masiya; anahitaji nguvu ya watu wengi, taasisi madhubuti na mikakati ya pamoja ili kuuangusha mfumo uliokita mizizi. La sivyo, tutajikuta tunaendelea kutazama sinema ya Lissu kama watazamaji wa kawaida, badala ya kuwa washiriki wa mabadiliko tunayoyatamani. Kwa hakika, Tundu Lissu peke yake hatoshi kuiondoa CCM madarakani. Kumbukeni maneno haya.
 
Tabia hii ya kutegemea mtu mmoja tu azungumze au kuchukua hatua inashangaza sana. Katika harakati za kweli za mabadiliko, kusema pekee hakutoshi, kunahitajika zaidi ya maneno.
Hata hivyo lazima tukubali kwamba jamaa ametupambania kweli weli
 
Yeye angesema wanaccm wenzake ni yupi aliyehoji. Halafu mauji ya mkuranga yalifanywa siri na serekali, kiasi kwamba hata wabunge wa upinzani walipotaka yajadiliwe bungeni, spika aliagizwa azuie huo mjadala.
BUnge lilelile watu wale wale.
 
Back
Top Bottom