Tabia hii ya kutegemea mtu mmoja tu azungumze au kuchukua hatua inashangaza sana. Katika harakati za kweli za mabadiliko, kusema pekee hakutoshi, kunahitajika zaidi ya maneno. Mfumo mbovu huondolewa na mfumo mbadala, si kwa kauli za mtu mmoja hata awe mashuhuri kiasi gani. Hizi hadithi za kila mara za kumtazama mtu mmoja kama mkombozi hazitatufikisha popote. Tundu Lissu si Masiya; anahitaji nguvu ya watu wengi, taasisi madhubuti na mikakati ya pamoja ili kuuangusha mfumo uliokita mizizi. La sivyo, tutajikuta tunaendelea kutazama sinema ya Lissu kama watazamaji wa kawaida, badala ya kuwa washiriki wa mabadiliko tunayoyatamani. Kwa hakika, Tundu Lissu peke yake hatoshi kuiondoa CCM madarakani. Kumbukeni maneno haya.