haya mambo ya kawaida kwa serikali yeyote, ninachoshangaa serikali yetu imeshindwa vipi kufanya usiri wa shughuli hii mpaka imevuja kwa wanaichi au ndio tunapungukiwa utaalam na vitendea kazi?
eneo la shughuli kunatakiwa kusiwe na aina yeyote na network ya kiraia kwa ajili ya mawasiliano angalau siku moja kabla ya shughuli kisha vijana wanaingia usiku wa manane kwa kushtukiza na kufanya kazi yao kwa ustadi wa hali ya juu sana.
Hii video haikutakiwa kufika hapa maana kwa mwanaichi wa kawaida ni vigumu kumuelezea hili suala akaelewa ndio maana hata kunakuwa na pande mbili za kupinga na kukubali ila huwezi pata suluhu na kusonga mbele bila kufunga mkanda na kujikaza kiume.
Vijana wametekeleza oda ya mkuu wao wa kazi hawana kosa lolote, uzembe mdogo waweza kua umejitokeza kwa waandaaji wa shughuli ndio maana wanasiasa wametumia mwanya japo walishaapa kuilinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwisho natoa pole kwa waliokumbwa na hii operesheni kimakosa.
**Ni mtazamo wangu tu, si kwa nia mbaya wakuu.