Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii thread imeniliza, tunaelekea wapi jamani?... Eeeh Mungu tunusuru...inasikitisha, inauma na inaudhi kuzidi maelezo. Inaonekana furaha yao watawala ni kuona watu wanauawa kila mahali nchini ili tuogope kuendelea kudai na ku-support mabadiliko, sidhani kama hawa police wanafanya ukatili na unyama huu bila maelekezo...kwa mwendo huu mabadiliko ni lazima. Inabidi kifanyike kitu kwa kweli..hii ni hatari.
hivi kweli hii ndio nchi niliyokuwa naipenda na kudiriki kusema kuwa sitakwenda popote. ipo wapi amani ya kweli ambayo kila siku viongozi wetu wanaihubir? ipo wapi demokrasia ambayo tunajisifu nayo katika mataifa mengine? uko wapi uhuru wa vyombo vya habari? wapo waliosema kuwa chadema ndio wanawaua wananchi je na hili la mwandishi wa habari aliyeuawa wakati anatafuta habri ni chadema tena? je kazi ya polisi ni kutuliiza maandamano ya wananchi pekee? mbona hatuwaoni wakiwashughulikia mafisadi na wezi wa rasilimali na mali zetu? nina maswali mengi sana ninajiuliza kuhusu nchi ya Tanzania lakini sipati majibu.....ninashawishika kusema kuwa Tanzania hakuna amani na serikali imejidhihirisha kama wauaji wa wananchi waliowachagua.... mnisaidie jamani
Tatizo sifa za kujiunga weng div 4 za 32 bora walimu div 4 za 28 hawa wadudu wakimuona ocd au rpc wanakimbia hao njaa bwana