Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Mwema na shemeji yako Kiwete ondokeni,ONDOKENI WAUAJI WAKUBWA;WAHUNI NA WABAKAJI WA DEMOKRASIA;ONDOKENI MAPEMA MADARAKANI MNANUKA DAMU ZA WATANZANIA.
 
Hii thread imeniliza, tunaelekea wapi jamani?... Eeeh Mungu tunusuru...inasikitisha, inauma na inaudhi kuzidi maelezo. Inaonekana furaha yao watawala ni kuona watu wanauawa kila mahali nchini ili tuogope kuendelea kudai na ku-support mabadiliko, sidhani kama hawa police wanafanya ukatili na unyama huu bila maelekezo...kwa mwendo huu mabadiliko ni lazima. Inabidi kifanyike kitu kwa kweli..hii ni hatari.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ipo haja kwa wanaharakati kuanza kampeni maalum ya kukusanya ushahidi wa majina husika ya polisi wanaoshiriki katika uvunjaji wa haki za binaadamu, kuweka record ya incidence zote pamoja na evidence kamili kwa wanayowatendea wananchi. Wajue iko siku watasimama mbele ya sheria kujibu mashitaka yao. days are numbered kwa hawa FFU wanaojifanya wako above the law, wamekosa utu na ihsani ya kuitwa polisi wanaolinda raia. Shame on you.
 
....Pole sana Mwasi....haya mapicha yanahuzunisha na kutia hasira sana. Naamini kabisa kama tutakuwa na mshikamano kukemea unyama huu unaofanywa nchini basi tunaweza kabisa kuukomesha ila tukiamua kunyamaza basi mauaji haya ya kutisha yatazidi kushamiri.

Hii thread imeniliza, tunaelekea wapi jamani?... Eeeh Mungu tunusuru...inasikitisha, inauma na inaudhi kuzidi maelezo. Inaonekana furaha yao watawala ni kuona watu wanauawa kila mahali nchini ili tuogope kuendelea kudai na ku-support mabadiliko, sidhani kama hawa police wanafanya ukatili na unyama huu bila maelekezo...kwa mwendo huu mabadiliko ni lazima. Inabidi kifanyike kitu kwa kweli..hii ni hatari.
 
Jeshi la polisi ni wauwaji na majangili..mwema na jk msipopelekwa the hague ntashangaa sana
 
ENZI ZA UKOLONI ASKARI WA KIKOLONI WAKIUA WALIKUWA WAKIPONGEZWA SANA HATA KUPANDISHWA CHEO.WAZEE WETU WALIPINGA UONEVU HUU MFANO,KING MKWAWA,na WENGINEO MWISHOWE WOTE WALINYONGWA KIKATILI MFANO CHIEF SONGEA.SITAKI KUJIAMINISHA KWAMBA SIKU ITATOKEA KAMA UKOLONI LEO WANANCHI KESHO NANI?IGP ANAteuliwa na nani?SITAKI TUWE KAMA RWANDA94.MISRI JE.mwisho, VYOMBO VYA DOLA VIPO CHINI YA WATAWALA(SERIKALI) WANA UHURU WA KUVITUMIA vizuri au vibaya.
 
Kutokana na mtiririko wa matukio ya kinyama yanayofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia nchini, ni dhahiri kabisa kwamba polisi wamepewa baraka zote. kama hivyo ndivyo, ina maana tayari kuna vita kati ya polisi na raia. Kama hali imefikia hapo kwa nini na sisi tusijibu mapigo tokea mitaani maana tunaishi nao?
 
Kwa hali ilivyo sasa wala sitashangaa wananchi wakiamua kufanya hilo
 
Hivi kweli hii ndio nchi niliyokuwa naipenda na kudiriki kusema kuwa sitakwenda popote?.

Ipo wapi amani ya kweli ambayo kila siku viongozi wetu wanaihubir?

Ipo wapi demokrasia ambayo tunajisifu nayo katika mataifa mengine?

Uko wapi uhuru wa vyombo vya habari?

Wapo waliosema kuwa CHADEMA ndio wanawaua wananchi, je na hili la mwandishi wa habari aliyeuawa wakati anatafuta habari ni CHADEMA tena?

Je kazi ya polisi ni kutuliiza maandamano ya wananchi pekee?,mbona hatuwaoni wakiwashughulikia mafisadi na wezi wa rasilimali na mali zetu?

Nina maswali mengi sana ninajiuliza kuhusu nchi ya Tanzania lakini sipati majibu.

Ninashawishika kusema kuwa Tanzania hakuna amani na serikali imejidhihirisha kama wauaji wa wananchi waliowachagua.
 
hivi kweli hii ndio nchi niliyokuwa naipenda na kudiriki kusema kuwa sitakwenda popote. ipo wapi amani ya kweli ambayo kila siku viongozi wetu wanaihubir? ipo wapi demokrasia ambayo tunajisifu nayo katika mataifa mengine? uko wapi uhuru wa vyombo vya habari? wapo waliosema kuwa chadema ndio wanawaua wananchi je na hili la mwandishi wa habari aliyeuawa wakati anatafuta habri ni chadema tena? je kazi ya polisi ni kutuliiza maandamano ya wananchi pekee? mbona hatuwaoni wakiwashughulikia mafisadi na wezi wa rasilimali na mali zetu? nina maswali mengi sana ninajiuliza kuhusu nchi ya Tanzania lakini sipati majibu.....ninashawishika kusema kuwa Tanzania hakuna amani na serikali imejidhihirisha kama wauaji wa wananchi waliowachagua.... mnisaidie jamani

Ni vizuri umejiuliza hayo maswali leo baada ya mzunguko kukufikia!
Ukweli ni kwamba hiyo nchi haipo na wala haijawahi kuwepo, kilichokuwepo na ambacho kipo ni propaganda tu za viongozi tangu mwanzo kujaribu kutuaminisha kwamba tunaishi ktk hiyo nchi uliyoielezea !

Jeshi la Polisi la Tanzania, kama vilivyo vitu vingi kwenye mfumo wetu, ni lile lile ambalo tumerithi kutoka kwa wakoloni, hatujabadilisha chochote kwa sababu ambazo watawala wetu wanazijua wao, kama ilivyo elimu yetu, kama zilivyo sheria tu nyingi kama sio zote, hivi unajua hata Sare tu za polisi bado zinatoka Uingereza mpaka leo?

Kwa kifupi Jeshi la Polisi au Jeshi la Wananchi (JWTZ) wamekuwa wakitesa na wakiua watu tangu ukoloni na mpaka leo sema tofauti tu ni kwamba labda sasa hivi mzunguko wa mauaji ya Polisi yamekufikia kwa hiyo unaona kama Tanzania uliyokuwa unaijua imebadilika, ukweli ni kwamba hamna jipya, kwetu kuna kambi ya Jeshi wanajeshi wakimaliza tu mafunzo breki ya kwanza Uraiani kupiga na kujeruhi na mara nyingi kuuwa raia, hiyo imekuwa ni kawaida, tangu mimi niko mdogo mpaka leo hii nimekuwa mtu mzima hakuna lililobadilka isipokuwa propaganda tuu!
 
Mauaji yanayoendelea kufanywa na polisi katika mikutano ya CHADEMA ya M4C ni njama ya Serikali kuwatisha wananchi ili wasishiriki mikutano hiyo kwa kuwa ni tishio kwa serikali. Vyanzo vetu vya habari vinaeleza kuwa huo ni mpango mahsusi ulioandaliwa ili kupata kigezo cha kupiga marufuku mikutano ya M4C.

Sasa kwa mtindo huu tutafika? Mimi nadhani vitendo hivi havivumiliki. Vinakiuka kabisa misingi ya utawala bora na demokrasia ambayo serikali yetu huwa ikijidai kuwa inafuata. Natoa wito kwa jumuiya ya Kimataifa kusitisha misaada yake kwa Tanzania kwa kuwa imesimamia ukandamizaji wa demokrasia na pia imeongoza mauaji na umwagaji damu wa wananchi wake.

Kama Serikali ipo basi ijibu tuhuma hii
 
Ndugu zangu watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii. Kwa takribani miaka minane sasa tumeshuhudia hali ya nchi ikizidi kudhoofu kiuchumi, maisha yamezidi kuwa magumu, hali ya elimu imekuwa ikishuka kiviwango, hali ya usalama wa raia imekuwa mbaya kiasi cha kufikia watu kuuawa na polisi hadharani. Kimsingi ni kwamba uongozi wa kisera umefikia tamati ya uwezo wake kifikra na uwajibikaji. Tuna wajibu mimi na wewe wa kurekebisha hali hii, na kuna namna nyingi za kukomesha mfumo kandamizi. Tulio wengi tungechagua mtindo wa mapinduzi ya umma. Njia hii ni nzuri na ina majibu ya haraka, lakini ina maumivu ya muda mrefu pia.

Nadhani tujadili njia ya kuidhoofisha serikali iliyoko madarakari, ambayo inapata nguvu kubwa kutoka kwetu wenyewe. Magari ya maji ya kuwasha, risasi, mabomu, fimbo, na zana zote za uhalifu wa utu wa mwanadamu zinatokana na kodi zetu. Matumizi ya anasa ya serikali yanatokana na kodi zetu.

Sasa ndugu watanzania, tunaweza kuiadhibu serikali yetu na ikatusikiliza iwapo tu tutainyima mapato. Na hili linawezekana pasipo kuvunja sheria yoyote ya nchi hii, tena ni njia yenye ufanisi wa hali ya juu na isiyo na madhara yoyote ya kiafya kwa tutakaoitumia.
Tuhamasishane kususia unywaji wa pombe na vinywaji jamii ya soda, tuhamasishane kususia uvutaji wa sigara. Hii ina madhara makubwa kwa mapato ya serikali, lakini si kwa uchumi wetu kama taifa, kwani kutatokea substitution effect, isiyo na madhara kwa uchumi lakini yenye madhara kwa serikali kikodi. Badala ya serikali kununua silaha za kupambana na wananchi wake, hicho kidogo itakachokipata italazimika kulipa mishahara ya watumishi wake.

Chaguo sahihi ni kunywa maji, na kula pipi kali (kwa wavuta sigara). Hii itadhoofisha serikali, hivyo itasikiliza kilio cha watu wake.
Napenda kusikia mawazo toka kwenu.
 
Polisi ndio chanzo cha mauaji yanayoendelea yakiwemo haya ya sasa ya Mwandishi wa habari Ndugu Daudi Mwandosi. Cha ajabu hao hao watuhumiwa NO. 1 ndio tumewaachia jukumu la kupeleleza na kuja na majibu ambayo sikuzote wametutaka tuyaamini nasi kwa umbumbumbu wetu tumekuwa tukiyaamini. Tangu jana nimekuwa nikifatilia mijadala kwenye blogs, social networks, tv, radio na kusikia kauli za wadau mbali mbali wengine viongozi wa vyama vyenye kukubalika wakihitimisha na usemi ule ule "TUNASUBIRI REPORT YA POLISI". Jamani TANGIA LINI FISI AKAKABIDHIWA BUCHA? KWA HILI TUSIWE MBUMBUMBU, TUTAKUFA-TUTAISHA!
 
Ukiangalia kwa makini picha zinazo muonyesha askari aliyeshikilia bunduki ya kurushia mabomu ya machozi na kumuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi iwapo huyu akifunguliwa mashitaka anaweza kujitetea mahakamani kuwa alikuwa anatekeleza amri "wanazo ziita halali". Je huyo RPC atakuwa tayari kufika na kutoa ushahidi kuwa amri ya kufanya hivyo ilikuwa yake?

Au haya yote yanatokea sababu ya upeo mdogo unaotokana na elimu ndogo waliyonayo askari wetu ya haki za binadamu ikiwemo ya darasani(nakumbuka walipokuwa wakija kufanya fujo chuo kikuu na wala siyo kutuliza fujo tuliwatania "Darasa la saba hao")? manake nakumbuka baada ya matukio ya mauaji ya raia kule Arusha baadhi ya mabalozi wanao wakilisha nchi zao hapa walishauri somo la haki za binadamu lisisitizwe kwenye mafunzo kule CCP(chuo cha polisi) au somo hilo lirudiwe upya kwa askari wote.

Nasema polisi hawa waangalie jinsi ya kutekeleza amri hizo sababu inapotokea mkono wa sheria kuingilia kati polisi huyo hufa lwake na wala hatomuona huyo bosi wake kama ni RPC au IGP wakija kumtetea. Polisi kumbukeni hawa wakubwa zenu wanatekeleza matakwa ya wanasiasa waliowaweka kwenye hivyo vyeo.

Nitakupeni mfano wa yatakayowakuta pindi hao mnao wapigania wakijikuta wako nje ya madaraka na mkono wa sheria kuwa juu yao; Kule Rwanda baada ya mauaji ya kimbari yaliyotokea 1994 askari wengi wamejikuta wanaishia gerezani na wengine wana kesi za kujibu baada ya kufanya mauaji kwa kutekeleza hizo amri wanazo ziita halali. Jiulizeni kwa nini hao walio watuma hawajaenda kuwatetea? Picha kama hiyo ndiyo inakuja Tanzania. Ipo siku hata kama ni baada ya miaka 30 wahusika watasimama kujibu.Kumbukeni habari za Pinochet Rais wa zamani wa Chile yaliyo mkuta baada ya miaka mingi kutoka madarakani. Kibaya zaidi hata alama za nyakati hamzioni, hao mnao watetea munauhakika 2015 wata survive?
 
Aaaaah!njaaa kaka,yaani njaa ndio inatufanya tutii kaposho kidogo tunaenda kupiga virungu na mabomu............alafu kwenye vurugu huwa tunapola simu na walet dah!...yaani we acha tu kaka...piga mabomu na risasi....njaaa mbaya kaka
 
Tatizo sifa za kujiunga weng div 4 za 32 bora walimu div 4 za 28 hawa wadudu wakimuona ocd au rpc wanakimbia hao njaa bwana
 
Tatizo sifa za kujiunga weng div 4 za 32 bora walimu div 4 za 28 hawa wadudu wakimuona ocd au rpc wanakimbia hao njaa bwana

wewe pimbi hivi mwalimu wa degree nae huwa ni division 4?omba chuo kikuu BAED na hiyoo division 4....ukipata nafsi nitajiunga ccm,kitu ambacha hakiwezekani.acha dharau kwa walimu
 
Back
Top Bottom