Huwa hamuwaelewi kwa sababu mmetanguliza uoga au chuki kabla ya kusikiliza na lugha.Na hata ukiegemea kwenye lugha,wao si waelezeaji wa jambo kwa kuremba na kunyambua kiundani kwa kila mtu.Kuhusu kutumia muda mwingi kwenye mazoezi hilo usibishe kabisa.Kazi yenyewe inahitaji waje kubishana na watu kuhusu "haki na ulaji" wa pilau kama mleta uzi. Unatarajia nini hapo?Polisi wanajengwa kutolewa tabia za kiraia wengine,uvumilivu,ukakamavu wa mwili,ujasiri,ubunifu,wepesi wa matumizi ya akili,utambuzi na ugunduzi,kuitangulia akili ya raia kimtazamo chanya,kuimiliki/kuimudu kazi na ikibidi kuishi kimaigizo bila kusahau heshima,utii na utunzaji siri wa hali ya juu.Hayo mambo hayahitaji dakika ishirini kwa siku.