Polisi inawakamata Waratibu wa LBL lakini Watu wanaendelea kupigwa hela kwenye mfumo huohuo

Mbona mimi naona kama jamaa aliweka hela tena 227,000/= ili aweze kulog in ili kutoa pesa, lakini ameletewa tena ujumbe kuwa bado wapo kweny majadiliano na BOT, pesa za wateja zitatolewa kwa pamoja
Watu wanapenda kujipa matumaini hewa, ndo imetoka hiyo
 
Mbona mimi naona kama jamaa aliweka hela tena 227,000/= ili aweze kulog in ili kutoa pesa, lakini ameletewa tena ujumbe kuwa bado wapo kweny majadiliano na BOT, pesa za wateja zitatolewa kwa pamoja
Waaminishe ujinga
 
Kuna story nikihadithia mtacheka sana!
Kuna kanisa la walokole wamepigwa kuanzia mchungaji hadi waumini.
Walitangaziwa kanisani🤣
Lbl wamepigwa wengi wengine hawasemi ila wamenuna balaa si shuleni si kazini si kanisani.
 
Sijui kwanini mamlaka hua zinaingilia kati haya mambo? Ifike kipindi tuache ili wapumbavu wapigwe hadi akili zikae sawa. Eti hadi leo watu bado wanaamini kuna kuweka hela na kupata faida mara tatu nne ndani ya mwezi 🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
Huu upumbavu wa LBL ni nini hasa? Inawahusu nani, ni DECI au uchafu gani inaitwa LBL?
 
Waaminishe ujinga
Nilikuwa nawafafanulia wagumu kuelewa ambao hawajamuelewa mleta mada.

Mleta mada nilivyomuelewa amepigwa mara mbili pesa yake na LBL.

Mara ya kwanza aliweka mzigo akashindwa kulog in, then LBL wamewataka wateja waweke hela ili waweze kulog in, ameweka hiyo 227,000/= then wanaambiwa wasubiri pesa zitatolewa kwa pamoja wapo kwenye majadiliano na BOT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…