Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 4,740
- 7,179
Mkataba upi mkuu?Hio kampuni si wameingia mikataba na makampuni ya simu yote si wayakamate makampuni ya simu nayo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkataba upi mkuu?Hio kampuni si wameingia mikataba na makampuni ya simu yote si wayakamate makampuni ya simu nayo
Watu wanapenda kujipa matumaini hewa, ndo imetoka hiyoMbona mimi naona kama jamaa aliweka hela tena 227,000/= ili aweze kulog in ili kutoa pesa, lakini ameletewa tena ujumbe kuwa bado wapo kweny majadiliano na BOT, pesa za wateja zitatolewa kwa pamoja
Maybe mtu kakopy ila ndio leo naona hiyo yenye underscore kaukweli....Jina na avatar ni sawa, unasema humjui🤔
Kama mawakala wao wa kulipa watu pesaMkataba upi mkuu?
Waaminishe ujingaMbona mimi naona kama jamaa aliweka hela tena 227,000/= ili aweze kulog in ili kutoa pesa, lakini ameletewa tena ujumbe kuwa bado wapo kweny majadiliano na BOT, pesa za wateja zitatolewa kwa pamoja
Lbl wamepigwa wengi wengine hawasemi ila wamenuna balaa si shuleni si kazini si kanisani.Kuna story nikihadithia mtacheka sana!
Kuna kanisa la walokole wamepigwa kuanzia mchungaji hadi waumini.
Walitangaziwa kanisani🤣
Mkataba upi na una ushahidi gani kwa hilo usemalo?Hio kampuni si wameingia mikataba na makampuni ya simu yote si wayakamate makampuni ya simu nayo
Hapana mfumo haupo hivi mkuuKama mawakala wao wa kulipa watu pesa
Sijui kwanini mamlaka hua zinaingilia kati haya mambo? Ifike kipindi tuache ili wapumbavu wapigwe hadi akili zikae sawa. Eti hadi leo watu bado wanaamini kuna kuweka hela na kupata faida mara tatu nne ndani ya mwezi 🚮🚮🚮🚮🚮🚮Licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa tangazo linaloeleza kuwa haihusiki na jambo lolote linalohusu Kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL) ambayo inavyoonekana kilio chetu ni cha Watu wengi, lakini nimeamua kuandika hapa kwa kuwa najua kuna wenzetu ambao wana msongo wa mawazo wanaendelea kama mimi wanaendelea kupigwa.
Ipo hivi wale ambao tulikuwa Wanachama, kila tukiingia kwenye mfumo huo kwa nia ya kuangalia nini kinaendelea, tunakutana na jumbe mbalimbali, mojawapo ni kuwa inatutaka kulipia hadi Tsh. 270,000 ili kuweza kuingia katika Akaunti husika na kufanya mchakato wa kunasua fedha zetu zilizokwama ndani.
Nafikisha ujumbe huu kupitia JamiiForums naamini ujumbe huu utafika sehemu nyingi kwa kuwa mimi siwezi kuwafikia BoT.
Ukifungua kwenye akaunti yako ya LBL kuna ujumbe ambao unakuja ukikuelekeza kulipa kulingana na kiwango cha fedha ambacho ulilipia wakati unajiunga.
Mfano levo ya P3 kiwango cha kujiunga ni Tsh. 540,000 hivyo unatakiwa kulipia nusu ya kiasi hicho ambacho ni 270,000 ili wakuwezeshe kufungua akaunti yako na uweze kutoa fedha zako zote zilizosalia kwenye Wallet uhamishe katika mitandao ya simu.
Kinachofanyika ni kuwa hasara inaongezeka kwa Watu kuendelea kuliwa zaidi licha ya juhudi nzuri za Serikali na Jeshi la Polisi linawakamata Watu.
Pia soma:
~ Jeshi la Polisi Morogoro lawakamata maofisa saba wa LBL kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha
~ Benki Kuu (BoT): Hatujatoa leseni wala kuruhusu shughuli za LBL
Nilikuwa nawafafanulia wagumu kuelewa ambao hawajamuelewa mleta mada.Waaminishe ujinga