Polisi, Jeshi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto mishahara yao ni midogo, Serikali muwaongezee

Polisi, Jeshi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto mishahara yao ni midogo, Serikali muwaongezee

Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi. Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.
Wanalipwa mshahara kiasi gani? Basic ni sh ngapi na take home sh ngapi? tuanzie hapo.Na je vyeo/ madaraja yao yanapandishwa baada ya muda gani na je wote wanapanda.Ni vema kuongea kwa data
 
Mishahara mikubwa sana kwako ni kiasi gani?
Nimesema JWTZ wana mishahara mikubwa kwa kulinganisha na kada nyingine nyingi za serikali.

Ukikuta mwanajeshi anajitambua, anapata maendeleo vizuri tu na hana njaa za ajabu ajabu!

JWTZ wanalipwa posho ya kila mwezi (laki 3), posho ya nyumba kama amepanga, kama ana degree basi degree inalipwa, wanawake wanapewa hadi hela ya pedi, posho ya vinywaji nk.

Ila mwalimu wa shule ya msingi ngazi ya cheto ambaye ndio muhimu sana kwani anatengeneza msingi wa wataalamu, takehome yake ni kama 280,000/= hivi, ambayo ni sawa na posho ya moja ya JWTZ.

Lakini huyu mwalimu anajikongoja hivyo hivyo kibishi mpaka anajenga kibanda, na maendeleo mengine. Ila mwanajeshi mwingine (siyo wote), yeye ni kuishi kwa mashindano, kunywa pombe chakari, wanawake nk. Anasema eti yeye atakufa siku yoyote kwa risasi, acha aponde raha!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi. Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.

Lazima maslahi ya wanawake kwenye majeshi hayo yafanane maana hapo unakutana na WP anakung’ang’ania ili uwe
Pesa anayoingiza askari mwenye elimu ya kidato cha nne au cha sita polisi, magereza au uhamiaji analingana na daktari mwenye degree aliyesoma miaka mitano kwa mkopo toka bodi ya elimu ya juu.

Mshahara wa askari wengi kwa vyeo vyakuanzia ipo hivi:
Take home kama 400,000
Posho 300,000
Hela ya vinywaji 100,000
Kama amepanga nje ya kambi analipwa hela ya pango kama 50,000
Jumla ni 850,000.

Daktari:
Take home baada ya makato yote ni kama 800,000.
Wakuonewa huruma hapo ni nani?
 
Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi. Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.
Hawahitaji huruma zetu kwa ssbabu wanakubali kutumika kubaka haki za binadamu na kushirikiana na CCM kuwaumiza wananchi.

Waishi kwa mishahara yao, tutakutana nao kwenye Katiba Mpya
 
Tumeanza na hao kuchokoza maada huko kuna madaktari MD analamba kama 800k hivi, manesi, walimu huko wanacheza na 400k hadi 600k hao nao wakuonewa huruma

Kuna watumishi wa umma hata afanye scrub vipi bado ngozi inakua imekakamaa sababu ya stress na mawazo hasa kwa hizo salary mfano maisha ya Dar anayamudu vipi ndio huchelewi kukuta watumishi wa umma nao wanajiuza kama kawaida tu
Wanagonga scrub hadi za maji ya betri lakini waaapiiii wamepaukaaaaaaa vijuso
 
Kiukweli kwa kazi kubwa sana za hayo majeshi. Wanafanya kazi kubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini maslahi yao hayaendani na kazi kubwa wanazozifanya.

Lazima maslahi ya wanawake kwenye majeshi hayo yafanane maana hapo unakutana na WP anakung’ang’ania ili uwe
Kwa nini hawasemi nakumbuka kulikuwa na mkubwa Moja police aliwahi kutoa kilio hichi hadharani miaka michache iliyopita akaishia kuchukuliwa hatua za kinidhamu
 
Back
Top Bottom