Mishahara mikubwa sana kwako ni kiasi gani?
Nimesema JWTZ wana mishahara mikubwa kwa kulinganisha na kada nyingine nyingi za serikali.
Ukikuta mwanajeshi anajitambua, anapata maendeleo vizuri tu na hana njaa za ajabu ajabu!
JWTZ wanalipwa posho ya kila mwezi (laki 3), posho ya nyumba kama amepanga, kama ana degree basi degree inalipwa, wanawake wanapewa hadi hela ya pedi, posho ya vinywaji nk.
Ila mwalimu wa shule ya msingi ngazi ya cheto ambaye ndio muhimu sana kwani anatengeneza msingi wa wataalamu, takehome yake ni kama 280,000/= hivi, ambayo ni sawa na posho ya moja ya JWTZ.
Lakini huyu mwalimu anajikongoja hivyo hivyo kibishi mpaka anajenga kibanda, na maendeleo mengine. Ila mwanajeshi mwingine (siyo wote), yeye ni kuishi kwa mashindano, kunywa pombe chakari, wanawake nk. Anasema eti yeye atakufa siku yoyote kwa risasi, acha aponde raha!
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app