Polisi: John Kohe aliingia benki na kumlazimisha mhudumu ampe fedha bila kufuata utaratibu

Polisi: John Kohe aliingia benki na kumlazimisha mhudumu ampe fedha bila kufuata utaratibu

Bila msukumo wa samia(laanatullah) polisi ni werevu na wenye uwezo wa kutumia akili zao vyema, jiulize, kama wameweza kulinda uhai wa mtu aliyejaribu kwenda kupora benki, na bado akajaribu kupambana na polisi ili kuwapora silaha, ambayo angeweza kuitumia vibaya dhidi ya polisi au raia wengine, sasa walishindwa nini kulinda uhai wa mama yule wa arusha asiyekuwa na madhara yoyote kwa polisi,raia,wala mamlaka? Hadi wakaona njia pekee ya kumfanya ashindwe kuishi na kulea familia yake ni kumtwanga risasi ya mgongo? Au walishindwa vipi kulinda uhai wa vijana wa mwanza waliokuwa wakiangalia zao mpira? Tena ndani? Hapa tukubaliane, tatizo ni samia( Mungu amlaani)
 
Walitakiwa wamtandike japo ya mguu au mkono
Kwanini wampige ya mguu au ya mkono wakati wahusika waliokuwa pale walishaona huyu tunamthibiti kwa nguvu zetu asilia?

Wenye mawazo kama haya ndiyo mkikabidhiwa vifaa vya hatari mnadhani ni vya kutumia mbio mbio bila kuzingatia hali ya tukio
 
Mtu huyo anaonekana anamatatizo ya Afya ya akili
wangempima kwanza kabla ya kumchukulia hatua nyingine
Niwape pengezi askari waliokuwa zamu kwa kutotumia silaha; kwani kutumia silaha ni hatua ya mwisho kabisa na hasa unavyobaini mtuhumiwa anakuzidi nguvu....silaha haitumiwi kizembe kama fimbo.
WAMEFUATA WELEDI WA MAFUNZO YA KIASKARI
Kuna wajinga wanasema eti kwanini hakupigwa hata ya mguu,yaani mtu ameonekana anadhibitika kiwepesi halafu tena silaha za moto zitumike?
 
Mtu yupo nyumbani kwake kafyatuliwa

Leo scene ya kifala kama hii ifanye wako na busara.! 🤭

Mbwa nyie na aliyewatuma kujisafisha 😎
 
Watanzania naona wamefika mbali sana ,
Nimeona video inasambaa mtandaoni inaonyesha askari akiwa amemshika Raia kama mtuhumiwa wametokea chumba kimoja wapo ndani ya bank

Wakati anamwongoza kutoka nje mara gafla yule Raia akataka kumpokonya askari silaha yake amtumia nguvu mpaka askari wenzie wakaja kumdhibiti huyo mtuhumiwa

Hichi kitendo kingeweza sababisha upotevu wa uhai either wa askari au Uyo mtuhumiwa

Namuonea huruma sana uyo jamaa maana kajikaanga si kidogo
Video ipo kwa page ya pastorkamugira sijui yule mwanaharakati
 
Kwa jicho lako la ndani unadhani jamaa angefanikiwa kumpora mjeda silaha angefanya nn, kwa hali inayoendelea hapa nchini na hasira walioyonayo vijana, tutarajie makubwa siku za mbeleni.
 
Mbona ata jamaa hawajamtandika na kitako cha bunduki sinema zetu
 
Mtu huyo anaonekana anamatatizo ya Afya ya akili
wangempima kwanza kabla ya kumchukulia hatua nyingine
Niwape pongezi askari waliokuwa zamu kwa kutotumia silaha; kwani kutumia silaha ni hatua ya mwisho kabisa na hasa unavyobaini mtuhumiwa anakuzidi nguvu....silaha haitumiwi kizembe kama fimbo.
WAMEFUATA WELEDI WA MAFUNZO YA KIASKARI
Wewe unazijua Sheria na Kanuni za Mafunzo ya Matumizi ya Silaha..
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya limetoa ufafanuzi kuhusiana na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Askari wa Jeshi la Polisi akipambana na mtu mmoja huku akiwa na bunduki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma Januari 19, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, tukio hilo lilitokea Januari 15, 2026 majira ya saa nane mchana katika Benki ya CRDB Tawi la Sirari, wilayani Tarime.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtu anayetajwa kwa jina la John Kohe Amosi, mkazi wa Kijiji cha Sokoni, Sirari, alifika katika benki hiyo akiwa na nia ya kutoa fedha licha ya kutokuwa na akaunti.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo aliingia ndani ya benki hadi eneo la wahudumu (bank tellers) akiwa amebeba begi dogo na kuanza kuwatishia kwa nguvu wahudumu akitaka apewe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.

Hali hiyo ilisababisha taharuki ndani ya benki, na askari waliokuwa zamu walilazimika kuingilia kati na kumtaka mtuhumiwa huyo atoke nje na kutii amri.

Hata hivyo, wakati askari alipokuwa akijaribu kumtoa nje, mtuhumiwa aliripotiwa kumvamia askari mmoja kwa lengo la kumpokonya silaha, hali iliyosababisha askari kutumia nguvu kumdhibiti na hatimaye kumtoa nje ya benki na kumtia mbaroni.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa hana akaunti katika Benki ya CRDB, na uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini nia yake halisi na kama alikuwa na mshirika au dhamira nyingine za kihalifu, kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

 
Back
Top Bottom