LGE2024 Polisi: Kada wa CHADEMA aliyefariki alipata ajali ya Bodaboda akiwa amelewa

LGE2024 Polisi: Kada wa CHADEMA aliyefariki alipata ajali ya Bodaboda akiwa amelewa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ni kawaida kwa jeshi letu kutoa taarifa kwa wakati.hususani kipindi na nyakati hizi za chaguzi ambazo upinzani hupenda sana kutoa na kuleta habari zenye kuleta taarifa. Kwa kufanya upotoshaji na uzushi
Taarifa ya kushambuliwa Lissu ilishatoka?
 
Tumeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii ikitolewa taarifa ya kutaka kuupotosha umma kuhusiana na kifo cha Joseph Remigius, Miaka 52 mkazi wa Kijiji cha Karagara, Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa ametia nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa sahihi ni kwamba Oktoba 31, 2024 Joseph Remigius majira ya saa tatu usiku akiwa anatoka kwenye Bar waliyokuwa wanakunywa pombe akiwa amebebwa na bodaboda walipata ajali na baada ya ajali hiyo walipata msaada na kufikishwa katika Kituo cha Afya Minziro na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Novemba 1,2024 majira ya saa kumi na dakika ishirini alfajiri ndipo zikapokelewa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Minziro kuwa Joseph Remigius amefariki dunia akiwa nyumbani kwake.

Hivyo hadi sasa kulingana na ushahidi wa mashuhuda wa ajali na waliompatia msaada na kumfikisha katika Kituo cha Afya Minziro, ajali ndiyo chanzo cha kifo chake. Endapo kuna mwenye ushahidi tofauti na huo wa mashuhuda wa ajali basi aufikishe Polisi ili ufanyiwe kazi.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Dodoma, Tanzania.

Pia soma ~ Missenyi, Kagera: Kada CHADEMA, Joseph Elemedius auawa akingojea Uteuzi kugombea Serikali za Mitaa
David Misime amekuwa Daktari wa kutoa taarifa ya chanzo cha ajali siku hizi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi la polisi Nchini limekanusha vikali taarifa za upotoshaji zinazoenea mitandaoni juu ya kifo cha kada wa CHADEMA aliyefariki Dunia .ambapo taarifa hizi za upotoshaji zinahusisha kifo chake na masuala ya siasa hasa kutia nia kwake.

Na hii ndio taarifa yake👎View attachment 3140830

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
Bado kuna watu wanaamini taarifa za polisi kwenye kifo cha mpinzani?
 
Kesi ya yule dc aliyemtindua bint wa watu marinda mpk kumtoa mbolea imeishia wapi

Ova
andikia uzi maalumu ili hatimae upate majibu ya kina ya msingi mrangi

kwasasa tuendelee kuwashauri na kuwatolea wito chadema waache pombe. Ni mbaya na zinawaharibu sana kwakweli 🐒
 
Tumeshuhudia kupitia mitandao ya kijamii ikitolewa taarifa ya kutaka kuupotosha umma kuhusiana na kifo cha Joseph Remigius, Miaka 52 mkazi wa Kijiji cha Karagara, Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa ametia nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa sahihi ni kwamba Oktoba 31, 2024 Joseph Remigius majira ya saa tatu usiku akiwa anatoka kwenye Bar waliyokuwa wanakunywa pombe akiwa amebebwa na bodaboda walipata ajali na baada ya ajali hiyo walipata msaada na kufikishwa katika Kituo cha Afya Minziro na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Novemba 1,2024 majira ya saa kumi na dakika ishirini alfajiri ndipo zikapokelewa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Minziro kuwa Joseph Remigius amefariki dunia akiwa nyumbani kwake.

Hivyo hadi sasa kulingana na ushahidi wa mashuhuda wa ajali na waliompatia msaada na kumfikisha katika Kituo cha Afya Minziro, ajali ndiyo chanzo cha kifo chake. Endapo kuna mwenye ushahidi tofauti na huo wa mashuhuda wa ajali basi aufikishe Polisi ili ufanyiwe kazi.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Dodoma, Tanzania.

Pia soma ~ Missenyi, Kagera: Kada CHADEMA, Joseph Elemedius auawa akingojea Uteuzi kugombea Serikali za Mitaa
Wale wapumbavu wa chadema waliokuwa wananipinga kuwa damu ngingi kumwagika wapo wapi ? Yu wapi mbowe yu wapi tundulisu wa wapi chadema ...hii damu mnayo shuhudia sasa ni tone tu labda mkubali kuwa chawa ndiyo salama yenu .....hivi chadema nzima kuna mtu mwenye asilimia hata 3 ya akili zangu kweli ?
 
David Misime amekuwa Daktari wa kutoa taarifa ya chanzo cha ajali siku hizi.
Unaambiwa marehemu alilewa kilabuni, alafu akapanda bodaboda saa tatu akapata ajari. Wasamalia wema wakampeleka kituo cha afya cha karibu, kule hakupewa rufaa akaruhusiwa kwenda nyumbani siku ileile. Alafu akafia nyumbani kwa ajari.

Kwahiyo sasa hivi wameamua wasiseme ni watu wasiojulikana, wameamua iwe ni ajari na ulevi.
 
Acha

Acha kuwa na mabezo
Kuwa na utu
Hizo siasa na vyeo vya watu visikutoe utu
Haya amekufa umefurahi kama utamla nyama
Ndizo siasa za CCM.
Nchi imetawaliwa na watu waovu.
Kuna tofauti ya watu waovu na watenda dhambi.

Watenda dhambi wanatubu mara kwa mara maana wanamuogopa Mungu.
Waovu hawamuogopi Mungu wala chohote . Wanaogopa kuuawa na kulogwa tu lakini wao kuua ni sawa, kuloga wengine sawa.
Waovu ni wafiraji, wasagaji, wanatoa makafara , wanapenda za majini n.k.

Siasa za CCM ni za chuki sana . Hawana tena utu zaidi ya madaraka na mali basi .
Viongozi wa dini wafuatilie maovu na mabaya makubwa wanayofanya CCM dhidi ya wapinzani na watangayika kwa ujumla ili wawaambie kweli waumini wao kuhusu laana kwa taifa lenye watawala waovu wanaonuka damu za watu na dhulma huku wakiwa wanapora mali za umma na kujilimbikizia wao na watoto wao.

Kanisa katoliki limeonyesha njia ya haki na kujitenga na dhulma za watawala wasiofuata sheria na haki.
KKKT limeainishwa na Askofu Shoo kutokana na mfumo mbaya wa kanisa hilo unaojenga madaraja bila kujali shida za wengine ndani ya kanisa hilo lisilo na mfumo wa Kitaifa zaidi ya kila Dayosisi kuwa na maslahi yake na KKKT kubaki kama picha tu isiyo na sauti wala maamuzi .
Mfumo unaowafanya wale maaskofu na wachungaji walioko kwenye Dayosisi zenye matajiri wenye uwezo wa kutoa sadaka nyingi kujisahau na kujiona kuwa wapo kwenye nchi yenye utajiri mkubwa na kuwasahau wale walioko kwenye Dayosisi na sharika zenye watu wa hali ya chini wakipambana na hali zao na wakati mwingine kukosa mpaka mishahara .
Shoo hajui kuwa kuna wachungaji na wainjilisti wa KKKT wenye maisha duni sana kutokana na hali ngumu ya waumini wao . Kuna wainjilisti hata baiskeli ya gia hawana achilia mbali pikipiki . Sasa yeye anaishi maisha ya hali ya juu kutokana na kuwa kwenye Dayosisi yenye mabilionea wa biashara za kila aina wenye uwezo mkubwa .
 
Unaambiwa marehemu alilewa kilabuni, alafu akapanda bodaboda saa tatu akapata ajari. Wasamalia wema wakampeleka kituo cha afya cha karibu, kule hakupewa rufaa akaruhusiwa kwenda nyumbani siku ileile. Alafu akafia nyumbani kwa ajari.

Kwahiyo sasa hivi wameamua wasiseme ni watu wasiojulikana, wameamua iwe ni ajari na ulevi.

Kuna siku nilisema kuwa Masuala ya kutafuta madaraka ni masuala ya Kiroho .
Huwezi kuwa mlevi kupindukia ,mzinzi kupindukia halafu ukafanikiwa kueka akili za watu kiroho. Watawaua wote na hamta wafanya kitu kwa sababu ya upumbavu.
Yaani kipindi kama hiki cha uchaguzi wa CCM kweli lihitu linakwenda kulewa kwenye Bar. Pumbavu sana .
Watawaua hata kwa sumu za panya blaliful. Yaani CCM walivyo na uchu wa kukaa madarakani waliache lijitu limelewa wakati ni tishio kwao. Kweli huo wema CCM wameanza lini?

CCM wameshasema kuwa hata Mungu hana maamuzi kwenye ushindi wao sasa bado tu Kuna majitu mapumbavu hayajajua tu kuwa kua vita kubwa kati ya wema na uovu. Kipindi hiki kilipaswa kuwa ni kipindi cha swala tano ,maombi ,kufunga, kusali sala ya Novena kama John Mnyika ili kumpa Mungu utukufu na ukuu wa kuweka watu wema madarakani .Kwa hali ilivyo ni wazi kuwa Wapinzani hasa Chadema hawajajua kuwa wamezingirwa na mbwa mwitu wakali. Bado wanajilegeza legeza kama vile hawaijui CCM.
 
20241102_122939.jpg

Rasmi kwa sasa Polisi Tanzania ni washirika wa watenda maovu dhidi ya upinzani!
Ni ngumu kuamini kwamba hospitali wanaweza kumruhusu mgonjwa wa ajali ambaye inaonekana madhara ya ajali yatasababisha kifo chake!
Polisi hawataki hata kufanya upelelezi zaidi wajue ajali ilihusisha watu wangapi, majina yao na zali zao.
Hawataki kujua hata chombo cha moto kina usajili upi na ni cha nani!?
I stand to be corrected!
 
View attachment 3141381

Siku hizi mtu akiwa anaumwa akafariki huwa tunatakiwa kuripoti polisi?

Napenda mnieleweshe
 
Kama niajali waweke taarifa iliyokamilika kuanzia usajili wachombo kilichosababisha umauti,dereva na sababu za ajali hiyo,,,Ili tulio karibu tukajilidhishe ,,,,na vipi kuhusu Hali ya dereva?? Nayeye Yuko wapi saizi Ili ajaribu kutuambia ilikuwaje ,,,,,mtu aliyepata ajali jana na akaruhusiwa kutoka hospital afu akafika home akafariki tunapaswa kupata majibu ya daktari tujue alimpima vipi na akajilizisha kuwa huyu mtu anaruhusiwa kutoka hospital afu ghafula tatizo ambalo dktr amesema limeisha linamuua mtu mara tu baada yakufika nyumbani,,,,,,,,,,MNAPOANDAA HIZO RIPOTI ZENU SIO KILA MTU NI CHAWA NCHI HII JITAHIDINI KUWA MAKINI KUNA UJINGA NA UTOTO mwingi kwenye hizo taarifa zenu
 
Back
Top Bottom