Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
TAARIFA KWA UMMA.
Nimefika kituo cha Polisi Mbweni kufuatilia hatma ya dhamana ya BAWACHA na mwanahabari wetu wa Mgawe Tv ndg. Harlod Shemsanga waliokamatwa asubuhi ya leo kwasababu ya kutokuwa na kibali cha kufanya Jogging.
Nimefika Mbweni Polisi saa 9:20 alasiri hii, mbele ya ofisi ya mapokezi kukawa na difenda lenye Maaskari Polisi na Wanawake wa CHADEMA ndani yake nimemtambua Mhe. Rose Mushi, Mhe. Lillian Kimei na wenzao wawili jumla wako wanawake wanne wa CHADEMA ndani ya difenda lile.
Nikawauliza ndg. Shemsanga yupo wapi?
Kimei akajibu : yumo mahabusu.
Nikauliza naona gari la Mhe. Ernest Mgawe hapa nje yupo wapi?
Kimei : Mgawe kaja kumfatilia Shemsanga kakamatwa yupo mahabusu, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kawe pia kaja kufuatilia hatma yetu kakamatwa pia yumo ndani mahabusu.
Nikauliza kulikoni watu wanaokuja kufatilia dhamana yenu wanakamatwa?
Kimei Akaniambia hata wewe wanakubeba muda sio mrefu.
Nimelazimika kujivuta pembeni kabla sijabebwa ili niwahabarishe juu ya kadhia hii ya Jeshi la Polisi kupoka uhuru wa Wanawake wa CHADEMA na watu wetu wa Mgawe Tv.
Difenda lililowabeba Wanawake wa CHADEMA limeondoka nao.
Mhe. Mgawe, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kawe na mwanahabari Shemsanga wapo mahabusu ya Mbweni Polisi.
Nasimama na PGO.
Naomba kuwasilisha.