Polisi KAWE mnatumika kisiasa. Kamwe hatukubaliani na mnayofanya

Polisi KAWE mnatumika kisiasa. Kamwe hatukubaliani na mnayofanya

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
TAARIFA KWA UMMA.

Nimefika kituo cha Polisi Mbweni kufuatilia hatma ya dhamana ya BAWACHA na mwanahabari wetu wa Mgawe Tv ndg. Harlod Shemsanga waliokamatwa asubuhi ya leo kwasababu ya kutokuwa na kibali cha kufanya Jogging.

Nimefika Mbweni Polisi saa 9:20 alasiri hii, mbele ya ofisi ya mapokezi kukawa na difenda lenye Maaskari Polisi na Wanawake wa CHADEMA ndani yake nimemtambua Mhe. Rose Mushi, Mhe. Lillian Kimei na wenzao wawili jumla wako wanawake wanne wa CHADEMA ndani ya difenda lile.

Nikawauliza ndg. Shemsanga yupo wapi?

Kimei akajibu : yumo mahabusu.

Nikauliza naona gari la Mhe. Ernest Mgawe hapa nje yupo wapi?

Kimei : Mgawe kaja kumfatilia Shemsanga kakamatwa yupo mahabusu, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kawe pia kaja kufuatilia hatma yetu kakamatwa pia yumo ndani mahabusu.

Nikauliza kulikoni watu wanaokuja kufatilia dhamana yenu wanakamatwa?

Kimei Akaniambia hata wewe wanakubeba muda sio mrefu.

Nimelazimika kujivuta pembeni kabla sijabebwa ili niwahabarishe juu ya kadhia hii ya Jeshi la Polisi kupoka uhuru wa Wanawake wa CHADEMA na watu wetu wa Mgawe Tv.

Difenda lililowabeba Wanawake wa CHADEMA limeondoka nao.

Mhe. Mgawe, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kawe na mwanahabari Shemsanga wapo mahabusu ya Mbweni Polisi.

Nasimama na PGO.

Naomba kuwasilisha.
 
Wewe hawajakukamata tu? Nenda kamsalimie Gaidi Mbowe kule Segerea.
 
Kuna roho isiyo ya KiMungu imelikumba taifa.

Labda ndani ya wanaotekeleza haya wapo sleeper agents wanahakikisha jamii inakorogeka haswaa.

Tusiache kuliombea Taifa na viongozi wake

Kinachoendelea kinatustua hata sisi CCM kindakindaki
 
Ifike wakati wapinzani Tanzania mzione huruma Familia zenu nyinyi hamna Mbunge hata mmoja ukiachana wale wa upendeleo natamani hata Mh.Mbowe akichomoka kwenye hii kesi achane na Siasa mnapigania kitu gani nyie mbona Watanzania wenyewe hawako tayari kaeni kimya mpaka wale mnao wasemea waseme Basi yatosha tunaingia barabarani kudai HAKI YETU.
 
Mtemi Hangaya aliwaambia mtulie hamutaki,mnamulaumu Nani?
 
Hao waliobebwa wamebebwa kwa sababu gani hasa;

1. Walikuwepo eneo la tukio?

2. Au ni kwasababu ni viongozi wa Chadema?

3. Sheria ya dhamana imekataza mtu anaefahamiana na mtuhumiwa either kutoka familia yake, au chama chake kumuwekea dhamana?

Haya matukio ndio yanayofanya polisi wazidi kuonekana ni tawi la CCM.

Bawacha nao sasa niwashauri, waache kuvaa hizo t-shirts za Katiba Mpya kwenye jogging yao, wavae t-shirts za kawaida kwasababu naamini mawazo ya Katiba Mpya sasa yako kwenye kila kichwa cha mpenda mabadiliko Tanzania.

Uwepo wa Bawacha kwenye hiyo jogging utawavutia wengi kushiriki na lengo litafikiwa la kufikisha ujumbe kusudiwa, wasiendelee kushindana na hawa polisi wanaojulikana dhamira zao.

Sasa waje tofauti ili kujua lengo hasa la polisi kuzuia hiyo jogging yao, kama wametumwa na CCM ijulikane, au kama sababu ni maandishi kwenye hizo t-shirts pekee ijulikane pia.
 
Kuna roho isiyo ya KiMungu imelikumba taifa.

Labda ndani ya wanaotekeleza haya wapo sleeper agents wanahakikisha jamii inakorogeka haswaa.

Tusiache kuliombea Taifa na viongozi wake

Kinachoendelea kinatustua hata sisi CCM kindakindaki
Amen
 
Ifike wakati wapinzani Tanzania mzione huruma Familia zenu nyinyi hamna Mbunge hata mmoja ukiachana wale wa upendeleo natamani hata Mh.Mbowe akichomoka kwenye hii kesi achane na Siasa mnapigania kitu gani nyie mbona Watanzania wenyewe hawako tayari kaeni kimya mpaka wale mnao wasemea waseme Basi yatosha tunaingia barabarani kudai HAKI YETU.
Umechemka! Ukae kimya ili?
 
Back
Top Bottom