Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Leo Julai 1, 2026 majira ya saa 10:00 asubuhi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limepokea taarifa kutoka kwa Ndugu Mrimi Zabron Mwita, mkazi wa Sirari na Katibu wa Mheshimiwa John Heche, kuwa walikwenda kwenye nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Ntahamba kwa lengo la kumwamsha mwenzao ambaye walimpigia simu kwa muda mrefu bila mafanikio ili waondoke kuendelea na ratiba yao.
Askari Polisi walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kuwakuta Mrimi Zabron Mwita pamoja na wafanyakazi wa nyumba hiyo. Walionyeshwa chumba ambacho inadaiwa alikuwa amelala mwenzao aitwaye Suezi Dani Maradufu.
Baada ya kukuta mlango umefungwa na kushindwa kumpata kwa njia ya simu, askari walilazimika kuvunja mlango. Walipofungua walimkuta Suezi Dani Maradufu akiwa amelala chini kifudifudi.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa ndani ya chumba hicho kulikuwa na dawa za binadamu za aina mbalimbali. Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni kwa uchunguzi zaidi.
Soma Pia: Dereva wa John Heche akutwa amefariki chumbani Kigoma
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali na limewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi huo ukiendelea.