Polisi kuua mlinzi wa bar Dar: Je, Chalamila anakwepaje kuwajibika?

Tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akivalia njuga wanawake wanaojiuza almaarufu makahaba. Zoezi lilianzia kwenye kuvamia na kuvunja vibanda maarufu vijjlikanavyo kama Vibanda vya Wahaya na kuwatia mbaroni baadhi yao.

RC Chalamila anayesifika kwa tabia za ufyatu ambapo aliwahi kusikika akisema kuwa akimkuta kibaka nyumbani kwake anamuua na hata aliwahi kusema hivi karibuni kuwa akiliamsha dude hakuna wa kumfanya lolote (hata sheria), amenadi kuwa ataendelea kuwasaka wanaojiuza miili yao kila kona ya mkoa wa Dar.

Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom (mlinzi wa bar hiyo aliuawa kwa risasi kutoka bunduki ya askari wetu), chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake wanawajibika na tukio hili la kinyama. Serikali inaendaje kuwasaka wanawake wanaojiuza kwa kutumia mtutu?

Chalamila ni mteule wa Rais, na kama inavyozoeleka mama huwalinda wale anaowapenda. Tunaamini kuwa Chalamila akiendelea kuwepo ofisini inapelekea jamii kuamini kuwa mteuzi anaridhika na mwenendo na maadili ya RC Chalamila.

Tunataka uwajibikaji na sheria ichukue mkondo wake kwa sababu maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa yamepelekea mauaji ambayo yangeweza kuepukika endapo busara zingetumika. Kuanzia muuaji na wote wanaohusika na sakata hili wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria ili haki ipatikanike.

Maadili ya viongozi wengi wa CCM imepelekea chama hiko kuwa kichaka cha wahalifu

Kwanza Sheria gani ya kuingia kwenye biashara ya mtu eti unasaka wanaojiuza,ina maana wakinikuta nimetoka na mpnz wangu na amevaa kimini wanambeba kisa kigezo ni kuvaa nguo fupi?
 
Accessory to crime.

Akili umeziazima, rudisha wakupe zako
Tuwe wakweli.Hata kama askari alikuwa anatekeleza maagizo ya wakuu wake sidhani kama aliambiwa akifika baa hiyo aanzishe ubishani na atakaowakuta(walevi) na wakizingua awatwange risasi.Huo ni ujinga wa askari mwenyewe/wenyewe.Hakubebewa akili wala kulazimishwa kwa vitisho aue.
 
Hili jiji ilivyo na matatizo mengi. Kweli unaenda kuhangaika kutafuta machangudoa bar. Yaani watu hawana kazi ya kufanya mpk unahangaika na miili ya watu. UKAHABA UPO TANGU MILELE HUKO ENZI NA PILATO. TENGENEZENI AJIRA NA MAZINGIRA mzuri ya biashara watu wataacha hayo mambo. We serikali ilikaa miaka 5 haijaajri then wanategemea watoto WA kike wapate wapi hela za pedi.
Ona Sasa bunduki na machangudoa mwisho mmemua mlinzi
 
Ripoti ya mwisho itakuwa huyo mlinzi wa bar alianzisha vurugu hadi kupelekea askari polisi kufyatua risasi hewani, lakini isivyo bahati ikamuua mlinzi huyo.

Nimemkumbuka sana binti Akwelina.
Kwa rekodi walizokuwa nazo hao jamaa wa mabatini hawachomoki

Ova
 
Mnalazimisha kesi siku zipite tu Hamna mambo ya kufanya? Mbona mnajisumbua tu..
 
Hili jiji ilivyo na matatizo mengi. Kweli unaenda kuhangaika kutafuta machangudoa bar. Yaani watu hawana kazi ya kufanya mpk unahangaika na miili ya watu. UKAHABA UPO TANGU MILELE HUKO ENZI NA PILATO. TENGENEZENI AJIRA NA MAZINGIRA mzuri ya biashara watu wataacha hayo mambo. We serikali ilikaa miaka 5 haijaajri then wanategemea watoto WA kike wapate wapi hela za pedi.
Ona Sasa bunduki na machangudoa mwisho mmemua mlinzi
Mkuu hizo ndio maksi za kupata vyeo ccm.
Huwezi kupata cheo kwa kutetea wananchi kwa mambo ya msingi.
Shida ya maji
Elimu
Miundombinu
Afya, haya hayana maksi kumpa mtu cheo.
Rejea asilimia kubwa ya viongozi wetu na jinsi walivyopanda hadi kupata nafasi za uongozi.
 
Tumeshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akivalia njuga wanawake wanaojiuza almaarufu makahaba. Zoezi lilianzia kwenye kuvamia na kuvunja vibanda maarufu vijjlikanavyo kama Vibanda vya Wahaya na kuwatia mbaroni baadhi yao.

RC Chalamila anayesifika kwa tabia za ufyatu ambapo aliwahi kusikika akisema kuwa akimkuta kibaka nyumbani kwake anamuua na hata aliwahi kusema hivi karibuni kuwa akiliamsha dude hakuna wa kumfanya lolote (hata sheria), amenadi kuwa ataendelea kuwasaka wanaojiuza miili yao kila kona ya mkoa wa Dar.

Juzi tu kumetokea mauaji mjini Dar es salaam kwenye Bar moja iliyopo Sinza iitwayo Boardroom (mlinzi wa bar hiyo aliuawa kwa risasi kutoka bunduki ya askari wetu), chanzo cha mauaji hayo yaliyofanywa na Askari Mbumbumbu ni kwenda kuwasaka makahaba hapo Bar!

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya mwenyekiti wake wanawajibika na tukio hili la kinyama. Serikali inaendaje kuwasaka wanawake wanaojiuza kwa kutumia mtutu?

Chalamila ni mteule wa Rais, na kama inavyozoeleka mama huwalinda wale anaowapenda. Tunaamini kuwa Chalamila akiendelea kuwepo ofisini inapelekea jamii kuamini kuwa mteuzi anaridhika na mwenendo na maadili ya RC Chalamila.

Tunataka uwajibikaji na sheria ichukue mkondo wake kwa sababu maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa yamepelekea mauaji ambayo yangeweza kuepukika endapo busara zingetumika. Kuanzia muuaji na wote wanaohusika na sakata hili wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria ili haki ipatikanike.

Maadili ya viongozi wengi wa CCM imepelekea chama hiko kuwa kichaka cha wahalifu

Pia Soma Boniface Jacob: Polisi walioua Mlinzi wa Bar ya Boardroom Sinza wadaiwa kutumwa na RC Chalamila kukamata Wanaojiuza
Kesha sema Polisi kuu mtu ni kawaida, bado nini.
 
Tuwe wakweli.Hata kama askari alikuwa anatekeleza maagizo ya wakuu wake sidhani kama aliambiwa akifika baa hiyo aanzishe ubishani na atakaowakuta(walevi) na wakizingua awatwange risasi.Huo ni ujinga wa askari mwenyewe/wenyewe.Hakubebewa akili wala kulazimishwa kwa vitisho aue.
Hebu tudadavulie mantiki ya kuwajibika.

Kosa huwa nanhatua kadhaa kabla ya kufikia kilele
 
Back
Top Bottom