Viongozi walio wengi ni wanafiki. Wanachokitenda siyo kilichopo moyoni mwao, ni usanii wa kutaka kujionyesha. Nenda kakague simu na computer zao utawakuta wamejaza picha za ajabu, lakini kwenye jamii wanajifanya watakatifu.Watanzania sijui wanatatizo gani na nguo fupi .... Yaani mwanamke kuvaa nguo fupi au suruali linawasumbua sana Wataznania wengi .... what's wrong with us. Watu wajue kuwa ni fashion tu na itapita. Huwezi mukuta mtu na kamin kake bar basi unaasume kuwa anajiuza .....!!
Tanzania si kisiwa, kwa utandawazi tulionao huwezi kuwachagulia watu mavazi. Je, huyo RC atafungia TV na mitandao dunia nzima watu wasione hayo mavazi mafupi? Hii tabia ya kuvamia nyumba za watu kwa kisingizio cha kuwasaka machangudoa siyo sahihi. Inawezekana kabisa hata yeye akawa miongoni mwa wateja wazuri wa hii biashara, maana machangudoa wapo kwasababu wanapata wateja.