Polisi kuua mlinzi wa bar Dar: Je, Chalamila anakwepaje kuwajibika?

Viongozi walio wengi ni wanafiki. Wanachokitenda siyo kilichopo moyoni mwao, ni usanii wa kutaka kujionyesha. Nenda kakague simu na computer zao utawakuta wamejaza picha za ajabu, lakini kwenye jamii wanajifanya watakatifu.

Tanzania si kisiwa, kwa utandawazi tulionao huwezi kuwachagulia watu mavazi. Je, huyo RC atafungia TV na mitandao dunia nzima watu wasione hayo mavazi mafupi? Hii tabia ya kuvamia nyumba za watu kwa kisingizio cha kuwasaka machangudoa siyo sahihi. Inawezekana kabisa hata yeye akawa miongoni mwa wateja wazuri wa hii biashara, maana machangudoa wapo kwasababu wanapata wateja.
 
Kumbe Chalamila ndio aliye fyatua risasai, 🥴🥴.
Aliwatuma askari akijua wanakuwaga na chamoto wakati dadapoa wanabebada kondomu tu, alishindwa nini kumtuma mtendaji wa mtaa akaenda na mgambo ambaye anafimbo tu,
 
Kauli ya RC Chalamila iliyochangia mauaji ya raia kule Sinza inalindwa na mamlaka ya uteuzi?

Kesi ya yule askari muuaji imeisha vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…