Polisi lawamani kwa mauaji Arusha - marehemu adaiwa kufariki na pingu mkononi. Mauaji mpaka lini?

Polisi lawamani kwa mauaji Arusha - marehemu adaiwa kufariki na pingu mkononi. Mauaji mpaka lini?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Yaani kwanini Jeshi la Polisi ??

Kijana Johnson Josephat ambaye shughuli yake inaelezwa ni kuuza vyuma chakavu mkazi wa mtaa wa Mulieti amefariki dunia katika mtaa wa Eso ambapo ameifanya kwa miaka 6 bila kupata tatizo lolote lakini amepatwa na umauti kwa kile kinachoelezwa ni mzozano ambao ulitokea kwa siku ya jana kutokana kupishana kauli na askari walikwenda kumkamata, huku yeye akitaka kwamba wamuonyeshe vitambulisho mvutano huo ukapelekea kushambuliwa kama wanavoeleza ndugu wa marehemu akiwemo mke na mama yake mkubwa.

Mama Mkubwa wa marehumu

Nilikuwa nipo nyumbani nimekaa nasikia watoto wamekuja kuniita wananiambia baba Jose anakibizwa huko na maaskari na mimi sasa nikawa na sikia kelele za mke wake nikatoka, kutoka naenda nikakuta ameshababizwa kwenye libanzi na ameigizwa kichwa sasa mke wake yupo hapo chini anawambia basi muachieni basi mbona mnampiga hivyo? wakawa awataki.

Kidogo nikawaambia watoto nendeni kamuite balozi naye balozi akaja na kuwauliza kwamba nyie kama mmekuja kumkamata kama anamakosa mimi ndiye balozi wake mbona amajafika kwangu? Nikawauliza mbona mnampiga hivyo na mtu mwenyewe huyu ametoka hospitali anatumia dawa.

Wakasema awajampiga nikawaambia mimi sinimeona kabisa mnavyofanya hapo mmemkandamiza kichwa mpaka mtu amekosa fahamu mpaka anaomba maji anasema msiniuwe na hapo hapo akakata fahamu.

Hivi mualifu si anakamatwa na kufikishwa Mahakamani jamani?. MTU anayepaswa kulinda Raia na Mali zake, ndiye anayeua Raia na kupora Mali zake. Watu wakambeba pale na kumpeleka hospitali, kumpeleka hospitali kule wakamkata wakasema huyu mtu mapigo yake ya moyo yameshuka sana anatakiwa apelekwe mount Meru au kwa babu.

Kijana mmoja akatoka hapo akasema ngoja tupige simu centro kwa sababu sisi tumeshashindwa hapa ili maskari wenyewe waje wampeleke Mount Meru ndiyo wakapiga simu na Polisi wakaja kumchukua na kumleta mpaka hapa nyumbani na wakamkalisha kama nusu saa nzima mpaka Mwenyekiti akaja na Mwenyekiti akawa anaongea naye na akampigia na Diwani baada ya hapo akapelekwa hospital lakini baada ya muda tukapewa taarifa ameshafariki dunia.

Mke wa Marehemu

Kuna mtu alikamatwa huko centro anavyodai huyo mtu aliiba complesa na akamuuzia yeye tulipofika eneo lla tukio nikawa nawaambia haya masuala ya kuongea na kama mtuhumiwa mnaye sitoonge kama hilo complesa lipo wakasema hatutaki kuongea sisi tunataka tumpeleke polisi. Wakawa wanapiga simu leteni gari ya polisi leteni gari ya polisi na walikuwa hawana hata vitamulisho wala nini.

Sasa tulipo mpeleka hospitali tukakataliwa kutibiwa kwa sababu alikuwa anapingu mkononi ikabidi wapigiwe maaskari wengine waje wamchukuwe wampeleke hospitali wenyewe kwa sababu wao si ndiyo walitumia maaskari wezao waje wamkamate kwahiyo wakaja maaskari wengine wakampeleka Mount Meru. Lakini wakati huo alikuwa ameshafariki.

Mbona wee Rais ni Mwanamke, mbona Wanawake Huwa Wana huruma na uchungu sana dhidi ya Uhai naomba ulitazame hili. Moyo wangu unaumia sana.

Soma Pia: Arusha: Afisa Upelelezi Omary Mahita akamatwa kwa tuhuma za kumvunja Mguu raia

Hivi mualifu si anakamatwa na kufikishwa Mahakamani jamani?.

Jeshi la Polisi Tanzania, wameua watu wangapi na kuwapora Mali zao ?.

MTU anayepaswa kulinda Raia na Mali zake, ndiye anayeua Raia na kupora Mali zake.

Katika Makosa aloyaruhusu Kuyafanya MAGUFULI na Yakamuondoa hapa Duniani Licha ya mazuri yake ni MAUAJI , NARUDIA MAUAJI .

Uhai ni zawadi ya Mungu Kwa mwanadamu, naye aliyeuleta Uhai huo ndio wa kuuchukua.

Ukijua, Utauliwa.

Mbona wee Rais ni Mwanamke, mbona Wanawake Huwa Wana huruma na uchungu sana dhidi ya Uhai .. nini kinekutokea?.

Hawa wapuuzi na wahuni, WALIOFELI kidato Cha Nne, wavuta mabangi, walojichomeka kwenye Jeshi la Polisi , ndo umeruhusu waendelee kufanya mauaji haya Kila siku??.

Yaani kwanini Jeshi la Polisi ?? Wao tuu Kila siku ?.

View: https://youtu.be/bIi_zbGwjYI?si=k4gEnQVTKZqCVkng

Moyo wangu unaumia sana.

Watakujibu mbona PK na M7 wameua sana na bado wapo?
 
Ni hatari sana , Mjinga Kua Kiongozi kwenye nafasi yoyote .

Hili Jeshi la Polisi, tukianza kufatilia Elimu zao, nitakua sahihi sana kua ni watu wenye Elimu ya kuunga unga Sanaa hali inayothibitisha, ujinga na ufinyu wa akili , automatically Wanakoswa Busara na weledi wa kazi.
 
Huyo muhalifu baada ya kufungwa pingu wenzake walijaribu kumtorosha na pikipiki akiwa na pingu akaenda kuanguka ndo sababu ya kifo chake
 
Hivi mualifu si anakamatwa na kufikishwa Mahakamani jamani?.

Jeshi la Polisi Tanzania, wameua watu wangapi na kuwapora Mali zao ?.

MTU anayepaswa kulinda Raia na Mali zake, ndiye anayeua Raia na kupora Mali zake.

Katika Makosa aloyaruhusu Kuyafanya MAGUFULI na Yakamuondoa hapa Duniani Licha ya mazuri yake ni MAUAJI , NARUDIA MAUAJI .

Uhai ni zawadi ya Mungu Kwa mwanadamu, naye aliyeuleta Uhai huo ndio wa kuuchukua.

Ukiua, Utauliwa.

Mbona wee Rais ni Mwanamke, mbona Wanawake Huwa Wana huruma na uchungu sana dhidi ya Uhai .. nini kinekutokea?.

Hawa wapuuzi na wahuni, WALIOFELI kidato Cha Nne, wavuta mabangi, walojichomeka kwenye Jeshi la Polisi , ndo umeruhusu waendelee kufanya mauaji haya Kila siku??.

Yaani kwanini Jeshi la Polisi ?? Wao tuu Kila siku ?.

View: https://youtu.be/bIi_zbGwjYI?si=k4gEnQVTKZqCVkng

Moyo wangu unaumia sana.

Utawaona watakavyo jikausha kama vile hawajui lolote
 
Huyo muhalifu baada ya kufungwa pingu wenzake walijaribu kumtorosha na pikipiki akiwa na pingu akaenda kuanguka ndo sababu ya kifo chake
Kwahiyo Polisi wenye SILAHA, wakamkamata, wakamtia Pingu.

Hapo hapo rafiki za Muhalifu wakafika ,wakiwa mbele ya Polisi wakataka kumtorosha Kwa Pikipiki huku Polisi wanashuhudia.

Hilo bichwa lako umelijaza UTAHIRA wa kiwango gani?.
 
Kuwa makini unavyotukana watu mtandaoni utakuja kumtukana kibenten wa mamaako
 
Back
Top Bottom