Polisi na TRA ni Taasisi mbili za Serikali ya Tanzania ambazo nazichukia kwa moyo wangu wote

Polisi na TRA ni Taasisi mbili za Serikali ya Tanzania ambazo nazichukia kwa moyo wangu wote

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Hapa nchini kwetu Tanzania, kuna taasisi mbili za serikali ambazo nazichukia kwa moyo wangu wote. Yaani taasisi hizi zingekuwa ni wanadamu nikaona wanaelekea kutumbukia katika shimo hatari na nisipowatahadharisha watakufa, ningekaa kimya ili wapotelee mbali.

1. Jeshi la Polisi Tanzania
2. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Hizi ni taasisi ambazo naona utendaj wake ni wa dhuruma, kukomoana, kuoneana, kubambikiziana, na kujiona wao ni miungu watu ambao wako juu sana ya Watanzania wengine, na ni haki yao kupewa rushwa.
 
Mimi Police hao siwapendi Sana
Ni vigumu sana kwa hapa Tanzania kujua tofauti kati ya Polisi na majambazi hatari. Angalau majambazi hawakumbakii kesi na kuomba rushwa, kwa hiyo labda majambazi ni nafuu, lakini wote wanaiba na kuua!

Binti yangu akija kusema naolewa na mtu askari Polisi au mfanyakazi wa TRA, itaniwia vigumu sana kumkubalia, japo wengine wataona kama binti anaolewa kwenye pesa nje nje ya rushwa kaukata kupata mume ambae atakuwa haishiwi!
 
Aaah, my friends there, I couldn't have said it better! Thank you very much.
 
Hawa jamaa wa Polisi na TRA nawachukia kiasi ambacho, binti yangu akija kusema naolewa na mtu askari Polisi au mfanyakazi wa TRA, itaniwia vigumu sana kumkubalia, japo wengine wataona kama binti anaolewa kwenye pesa nje nje ya rushwa!

Nimeshangaa kuona kuwa kumbe hata enzi za Kibiblia walichukiwa kama ninavyowachukia mimi leo, na makosa yao ni yale yale ya toka enzi hizo, utendaj wake ni wa dhuruma, kukomoana, kuoneana, kubambikiziana, na kujiona wao ni miungu watu
 
Hivi polisi mlipata laana gani
Mtu ukiwa karibu au rafiki na polisi jamii lazima ikutenge tu..inajua unawasinich😂

Pwolisi badilikeni dunia tuliyo nayo sio kama enzi za mkoloni.
 
Kama mpaka Mstaafu wetu Paul Makonda naye ameanza kuwalalamikia Polisi, kweli siyo watu wazuri...
Screenshot_20220313-085131.jpg
 
Ni vigumu sana kwa hapa Tanzania kujua tofauti kati ya Polisi na majambazi hatari. Angalau majambazi hawakumbakii kesi na kuomba rushwa, kwa hiyo labda majambazi ni nafuu, lakini wote wanaiba na kuua!

Binti yangu akija kusema naolewa na mtu askari Polisi au mfanyakazi wa TRA, itaniwia vigumu sana kumkubalia, japo wengine wataona kama binti anaolewa kwenye pesa nje nje ya rushwa kaukata kupata mume ambae atakuwa haishiwi!
Balaa kaka nina jamaa tulisoma nae ni Askari police siku mpaka nilimwambia nyie askari siwapendi sana kuna mwingine lilikujaga kunikamata siku nmekutana nalo nililia buyu vibaya
 
Hivi polisi mlipata laana gani
Mtu ukiwa karibu au rafiki na polisi jamii lazima ikutenge tu..inajua unawasinich😂

Pwolisi badilikeni dunia tuliyo nayo sio kama enzi za mkoloni.
Ukiniambia una urafiki na askari POlisi kama tulikuwa marafiki hapo ndio mwisho wa urafiki wetu. Zamani nilimuona POlisi kama mtu shujaa wa kupambana na wahalifu, lakini sio siku hizi. Namumuona POlisi kama jambazi ambae atakuua bila hurua au kukubambikiza kesi ili afaidike na kitu fulani.

Mtizamo wangu usilumiwe kwa sababu kuna Polisi wachache sana walio safi, lakini hao huenda ni asilimia 3% ya jeshi lote la polisi. KUanzia juu hadi chini, Polisi wetu ni uozo mtpu.
 
Kama mpaka Mstaafu wetu Paul Makonda naye ameanza kuwalalamikia Polisi, kweli siyo watu wazuri... View attachment 2148605
HUyu Makonda ndio usimsikilize kabisa!

HUyu ndie Marekani walisema ANA HATIA YA KUWANYIMA WATU HAKI ZAO ZA KUISHI, na maana ya maneno hayo ni kwamba, ana hatia ya kuua watu.

KIla mtu sasa anajua nani aliongoza kikosi cha Wasiojulikana, kwa hiyo nani alisimamia utekaji na uuaji wa Watanzania kwa kuwa tu waliikosoa serikali. Na tunajua pia POlisi walikuwa wanakataa kuchunguza hizo kesi zote na kutoa majibu ya kujiumauma kila walipoulizwa kwa sababu walijua ni nani wailokuwa nyuma ya Wasiojulikana na kwa amri ya nani
 
Hahahaha! Mkuu NIDA wao angalau hawabambikii watu kesi. Tatizo la NIDA ni uongozi mbovu tu na uzembe, na pia kwa kiasi fulani kutopewa fedha za kutosha na serikali

Ningekuwa mchawi wa kwanza kumrogo angekuwa Polisi - namuondoa mdomo na macho ili aache kuomba rushwa na kuua watu wasio na hatia.

Wa pili kumroga angekuwa TRA, namfanya asipate choo mwaka mzia ajae uchafu wake wa uonevu na rushwa huko tumboni hadi akome
 
Ni vigumu sana kwa hapa Tanzania kujua tofauti kati ya Polisi na majambazi hatari. Angalau majambazi hawakumbakii kesi na kuomba rushwa, kwa hiyo labda majambazi ni nafuu, lakini wote wanaiba na kuua!

Binti yangu akija kusema naolewa na mtu askari Polisi au mfanyakazi wa TRA, itaniwia vigumu sana kumkubalia, japo wengine wataona kama binti anaolewa kwenye pesa nje nje ya rushwa kaukata kupata mume ambae atakuwa haishiwi!
Basi muoe wewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tena hao polisi kuna mida wanafanya hadi kazi za TRA.

Tuendelee kukwepa kodi maan maendeleo yenyewe ya machale
 
tatizo polisi kuna wakati wanatumika vibaya, kuna siku tumepishana maneno na mpuuzi mmoja hapo hapo akaita polisi kuwa namfanyia fujo ilhali nilimwambia mbona nipo kwenye foleni wanahudumiwa wengine bila kufata utaratibu wa aliekuja kwanza, dah nashukuru tu huyo Kinega wake alikuwa mbali ndio nikanusurika ina maana angekuwa karibu lazima angechangamkia maana anajua akikuweka ndani ashapata hela, kwenye maisha haya ya TZ usipokuwa kwenye system au ndugu kitengo hata kwenye haki yako unaweza teseka bila sababu, dah inasikitisha sana.
 
Hapa nchini kwetu Tanzania, kuna taasisi mbili za serikali ambazo nazichukia kwa moyo wangu wote. Yaani taasisi hizi zingekuwa ni wanadamu nikaona wanaelekea kutumbukia katika shimo hatari na nisipowatahadharisha watakufa, ningekaa kimya ili wapotelee mbali.

1. Jeshi la Polisi Tanzania
2. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Hizi ni taasisi ambazo naona utendaj wake ni wa dhuruma, kukomoana, kuoneana, kubambikiziana, na kujiona wao ni miungu watu ambao wako juu sana ya Watanzania wengine, na ni haki yao kupewa rushwa.
Hakika wewe umenena
 
Bunge na wabunge ambao wengine wanajua tu kusoma na kuandika wanahusika kwa sehemu kubwa na miswada inayokuja kuwa sheria.

Wanasheria wanasoma miaka minne ili waje kuifanyia kazi sheria ambayo inatokana na bunge ambalo lina watu wanaojua kusoma na kuandika.

Polisi wanaisimamia sheria isivunjwe wengi ni form four. Tuache lawama.
 
Back
Top Bottom