Polisi Njombe: Mwanaume aliyeua Mkewe na Kumkata Vipande Vipande Alinyimwa Unyumba

Polisi Njombe: Mwanaume aliyeua Mkewe na Kumkata Vipande Vipande Alinyimwa Unyumba

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amesema Tumaini Luvanda (35) Mkazi wa Dombwela Wilaya ya Makete Mkoani Njombe aliyeuawa kwa kukatwakatwa na panga vipande na kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, na baadhi ya viungo vyake kutupwa Mtoni katika eneo la Kabinda Wilayani humo, ameuawa kutokana mgogoro wa ndoa na Mume wake kwasababu ya kumnyima unyumba Mumewe.

Amesema mara baada ya kumkamata Mtuhumiwa Juma Kyando (36) ambaye ni Mume wa Tumaini (Marehemu) kwa kuhusika na mauaji hayo wamebaini kuwa Familia yao ilikuwa na matatizo ya ndoa kwa muda mrefu ambapo Mwanaume amekuwa akinyimwa unyumba lakini pia siku aliyotekeleza mauaji hayo Mke wake alichelewa kurudi nyumbani.

“Familia hii ilikuwa na tatizo la ndoa kwa muda mrefu na Mwanaume amekuwa akinyimwa unyumba na siku hiyo ya tukio Mwanamke aliondoka nyumbani na alichelewa kurudi alipohojiwa na Mume wake hakuwa na maelezo mazuri jambo ambalo lilimpandisha hasira Mumewe na kutekeleza tukio hilo, niueleze tu umma Mtu huyu tumemkamata na tunakamilisha upelelezi ili tuweze kumifikisha Mahakamani”

Hata hivyo Kamanda Banga amesema kwa namna Mtuhumiwa alivyokuwa akitekeleza tukio hilo imeonesha uwezo wake wa kufikiri ulikuwa ni mdogo hali inayowafanya waendeleee na uchunguzi wa kidaktari ili kuona kama alikuwa mzima wa afya wakati akitekeleza tukio hilo.

- Njombe: Juma Kyando, adaiwa kumuua mke wake kisha kumkata vipande na kwenda kumtupa mtoni
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amesema Tumaini Luvanda (35) Mkazi wa Dombwela Wilaya ya Makete Mkoani Njombe aliyeuawa kwa kukatwakatwa...
Kizazi cha nyoka chenye ubinafsi, husda, chuki, visasi, uzandiki, dharau, masimango matambiko, ulozi, na kila aina ya ushetani...[emoji2960]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
kumbe marehemu alikuwa na makosa,

Kama mmesha anza kumtetea mapema hivi,hata adhabu yake itakuwa ndogo sana.
 
Back
Top Bottom