Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia padre Jordan Kibiki wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mafinga, kwatuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana. Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amethibitisha kukamatwa kwa padre huyo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakutekwa bali ametoa taarifa hizo za uongo kupitia mtandao wa WhatsApp, akidai alitekwa na kupelekwa jijini Mbeya kwa kutumia gari aina ya Toyota Alphard, na kwamba mmoja wa watekaji alikuwa na bastola.
Kamanda Bukumbi amesema kwamba baada ya taarifa hiyo kuchapishwa, baadhi ya mapadre wenzake walienda kutoa taarifa za kutekwa kwa Padre huyo katika Kituo cha Polisi Mafinga tarehe 18 mwezi wa tisa. Aidha, uchunguzi umebaini kuwa Padre huyo alikuwa anakabiliwa na madeni makubwa baada ya kukopa fedha kutoka kwa watu mbalimbali na kushindwa kurejesha. Katika hatua nyingine, jeshi hilo pia linawashikilia watu watano kwa tuhuma za utakatishaji fedha na udanganyifu kupitia mwamvuli wa dini.
===============
Hii taarifa hadi watumishi wa bwana wamegeukwa au ni kutokana na taarifa ya Mange ya hivi karibuni kuhusu barua iliyovuja ya Serikali kutoa maagizo ya kuwatambua Viongozi wa Dini wasiomuunga mkono Rais Samia. Au jamaa alikuwa kwenye orodha nini?