Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Aloooo jamaa walimteka bana! Taarifa ya polisi inasema walimchukua tar 15, Feb na siku hiyo hiyo ndio akachukuliwa kwenye kwenye mashtaka
hata bila D mbili hesabu hii haiwezi kukushinda.
Halafu eti familia yake iliruhusiwa kumuona juzi, na leo amerejeshwa kwenye kituo chake kuendelea na kazi. Jamaa kilimramba!
Kwa taarifa hii ya Polisi inamaanisha imebidi tu wamshataki ili kuua soo, kelele za wananchi ndo zimesaidia hadi kaachiwa!
KWanini tuwe na wezi, majambazi na wauaji wakati tupo na Polisi dhalimu?🌚🌚
Nafikiria hata yule jamaa aliyesema walipewa kazi na CCM Oktoba 29 kama naye atakuwa salama au ameshaoza tayari!
======
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Nassoro Mana, ametekwa, likieleza kuwa askari huyo yupo salama na anaendelea na majukumu yake ya kazi.
Pia soma: Polisi ataka kumpasua RPC wa Pwani hadharani Waziri Mkuu amzuia
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lingependa kueleza kuwa taarifa hiyo si ya kweli na ufafanuzi wake ni kwamba askari huyu alikuwa Mkoa wa Tanga akihudhuria mashtaka ya kijeshi kuanzia tarehe 15.02.2026 mpaka yalipokamilika na kutumwa kwenye mamlaka yenye maamuzi juu yake.
Aidha, Familia ya Mkaguzi huyo wanafahamu suala hilo kwani Mke wake aitwaye Hawa Msuya, alifika Mkoani Tanga na kuonana na mumewe. Tarehe 08.04.2026 mkaguzi huyo alipewa kibali cha safari (Movement Order) kutoka Mkoa wa Tanga kwenda kuripoti Polisi Mkoa wa Pwani ambako ndio kituo chake cha kazi. Tarehe 10.04.2026 majira ya saa 4:00 asubuhi Mkaguzi huyo ameripoti Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na kuelekezwa kurejea Polisi Wilaya ya Chalinze kuendelea na majukumu yake ya kazi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa rai kwa wananchi, Waandishi wa habari kutotumia vibaya mitandao ya kijamii na vyombo vyao vya habari kwa kutoa taarifa za uongo na kuleta taharuki kwa wananchi na viongozi. Aidha hatua kali kwa mujibu wa sheria zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakayekiuka sheria, kanuni na taratibu.
Waandishi wakitangaza kuhusu habari ya Afande kutojulikana alipo
Aloooo jamaa walimteka bana! Taarifa ya polisi inasema walimchukua tar 15, Feb na siku hiyo hiyo ndio akachukuliwa kwenye kwenye mashtaka

hata bila D mbili hesabu hii haiwezi kukushinda.Halafu eti familia yake iliruhusiwa kumuona juzi, na leo amerejeshwa kwenye kituo chake kuendelea na kazi. Jamaa kilimramba!