PreGE2025 Polisi Tabora: Aliyemuomba msamaha Heche sio Polisi, tayari tumeshamkamata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limesema kwamba, halina Mkuu wa kituo cha polisi wa aina ya yule ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari kisemacho "Mkuu wa kituo cha polisi Tabora amuomba msamaha Heche baada ya vurugu", na kwamba tayari limemkamata mtu huyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao, na kuwataka wananchi waipuuze picha mjongeo hiyo kwani imetengenezwa kwa lengo la kuwahadaa na kuwapotosha.

Soma Pia: Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabora amuomba radhi John Heche kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa CHADEMA

"Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora halina Mkuu wa Kituo cha Polisi Igunga wa aina hiyo, na kutokana na kitendo hicho cha kihalifu cha kutengeneza na kusambaza taarifa ya uongo,Jeshi la Polisi limefanya msako na kufanikiwa kumkamata mtu aitwaye Daud Paul Delim (49), ambaye ni mkazi wa Mbagala A wilayani Igunga aliyejifanya ni Mkuu wa Kituo cha Polisi akiomba msamaha, amekamatwa na anaendelea kuhojiwa ili kujua alioshirikiana nao kuandaa picha mjongeo hiyo hasi na potofu na kuisambaza ili hatua stahiki za kisheria dhidi yao zichukuliwe," imeeleza taarifa ya RPC Tabora

Source: East Africa TV
 
Wakuu,

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limesema kwamba, halina Mkuu wa kituo cha polisi wa aina ya yule ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari kisemacho "Mkuu wa kituo cha polisi Tabora amuomba msamaha Heche baada ya vurugu", na kwamba tayari limemkamata mtu huyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao, na kuwataka wananchi waipuuze picha mjongeo hiyo kwani imetengenezwa kwa lengo la kuwahadaa na kuwapotosha.

Soma pia: Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabora amuomba radhi John Heche kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa CHADEMA

Anadhihirisha kuwa polisi hata siku moja hawawezi kuomba samahani kwa Chadema
 
🐼🥷
1000036081.jpg
 
Hii nchi bhana....
 
Back
Top Bottom