Polisi Tanga: Askari Mwita alifariki kwa Kujinyonga, Uchunguzi unaendelea

Unajua huyu inawezekana kuuawa kwake kuna uhusiano na mauaji ya 29/10? Inawezekana kabisa alikuwa shahidi muhimu au alitoa ushahidi kwa watu wa Nchimbi hasa kuhusu watu waliozikwa kwenye makaburi ya jumla.

Haswaaa, sasa hivi wanatafutwa polisi wote wanaopinga na maamuzi ya Oct 29, ni mwendo was kuwamaliza tu.
 
 

Attachments

  • 1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 7
  • IMG-20260827-WA0003.jpg
    82 KB · Views: 7
  • IMG-20260829-WA0027.jpg
    326.2 KB · Views: 9
Haiwezekani mahabusu ajinyonge akiwa ndani ya selo ambayo ina mahabusu wengine, kufa kwa kukosa hewa si conclusion halisi kwani hata akikabwa au akinyongwa matokeo ni yaleyale sawa na ya kujinyonga. Ndugu zake wanadai ameng'olewa kucha na meno, ametobolewa macho na ameingizwa chupa kwenye tundu la haja kubwa(assuming the family is telling us the truth) je yote hayo amejifanyia mwenyewe?
 
Sorry to say,
Ila mi naonaga police majority watu fulani wasioweza kbs kufanya vitu kwa weredi, mission zao zimekaq kijinga jinga kama watu wasio watalaam katika eneo hilo.

Anyway nina maswali yangu kwa
RPC, IGP na Waziri wa Mambo ya ndani;
1. Alijinyonga kwa kutumia kitu gani, na kiko wapi kama ushahidi?

2. Kama mahabusu walikuwa watu sita, kwa nini hakuna aliyegundua mapema hata kuhusi purukushani za mtu akiwa katika hali ya kukata roho, sawa mahabusu walichoka, what's councidence mahabusu wote walale usingz wa pono na kupitiwa kiasi cha kushindwa kusikia purukushani za mwenzao akiwa anagangaika kukata roho, au ni mtu pekee aliyefanya suicide na kujinyonga kimya kimya Imekaaje hii?

3. Kama kuna CCTV za kituo zinaonyesha nini kabla na wakati wa tukio?

4. Nani alikuwa na ufunguo na access ya chumba cha mahabusu?

5. Forensic imewezaje kuthibitisha kuwa ni kujinyonga na si kunyongwa?

6. Post-mortem imebaini majeraha gani mengine mwilini?

7. Je, mwili ulifanyiwa toxicology ili kujua kama alikuwa ametumia dawa/sumu au kitu kingine?

8. Kwa nini taarifa ya kifo imechelewa kutolewa, licha ya tukio kutokea tarehe 27 Agosti?

9. Kwa nini uchunguzi wa kifo unafanywa na mfumo huo huo uliokuwa unamshikilia marehemu na ambao ndani yake wapo watyhumiwa wengine?

10. Je, Serikali iko tayari kwa uvhunguzi huru ukihusisha kuchunguzwa kwa OCD, OC CID, RPC, IGP na Waziri wako tayari kwa uchunguzi huru wa forensic na kuweka matokeo wazi?

Assumptions 5 za Kuchunguzwa
Custody failure:

1. Je, taratibu za ulinzi wa mahabusu zilikiukwa kwa mujibu wa PGO?

2 Scene contamination: Nani aliingia eneo la tukio wa kwanza?

3. Cause of death: Je, ushahidi wote unaendana na kujinyonga?

4. Evidence integrity: CCTV, nguo, ligature na samples zilihifadhiwa vizuri, kama haukuhifadhiwa vzr kwa nn nani anawajibika?

5. Unexplained injuries: Kucha, macho au majeraha mengine ni kweli yapo, na yalisababishwa na nini?

Kesi hii haihitaji hitimisho la haraka; inahitaji ushahidi unaoweza kuthibitishwa.
 
nimejifunza kitu hapa
 
Haya ndio matunda ya MO29 soap, wacha wafu wazikane.

Kuna wengine hapa wanamjadili Nchimbi hali alijiuzulu mwenyewe, nashauri wapigwe marufuku pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…