Polisi Tanga: Askari Mwita alifariki kwa Kujinyonga, Uchunguzi unaendelea

Polisi Tanga: Askari Mwita alifariki kwa Kujinyonga, Uchunguzi unaendelea

View attachment 3660766
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linapenda kutoa taarifa kuhusu kifo cha askari namba. H.1796 Koplo Mwita, aliyekuwa akishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi katika kituo cha Polisi Wilaya ya Tanga.

Tarehe 27 Agosti 2026 majira ya saa moja na dakika tatu usiku, askari huyo alikutwa akiwa amefariki dunia ndani ya chumba cha mahabusu katika kituo hicho

Kabla ya kifo chake, marehemu, pamoja na Afisa mmoja na Askari watano wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali, walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai.

Kufuatia kifo cha askari huyo, uchunguzi wa kisayansi uliofanyika na ndugu zake kushuhudia ulibaini chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga.

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linatoa rai kwa baadhi ya Wananchi,baadhi ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuandaa na kusambaza taarifa zisizothibitishwa au kutoa hitimisho lisilotokana na matokeo rasmi ya kiuchunguzi, kwani kwa kufanya hivyo ni upotoshaji ambao ni kinyume cha sheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kuwa uchunguzi wa tukio hili unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia taratibu zote za kiuchunguzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Imetolewa na

Kamanda wa Polisi. Mkoa wa Tanga

MY TAKE

Polisi anawezaje kujinyonga Mahabusu huku kukiwa na watu wengine watano?

Wanadai uchunguzi umebaini alikosa hewa. Kwanini hakukosa hewa kabla ya kutuhumiwa hayo makosa ya Jinai?

Je, ni nani alimn'goa kucha na kumtoboa macho?

Ukweli utajulikana na sisi tutazidi piga kelele.

Kumbuka kifo kilitokea 27/08.2027 jioni wakauchuna kutoa taarifa wakijua litapita. Baada ya watu kupiga kelele ndo tarehe 31/08/2026 jioni wametoa taarifa huku wakikataza watu kujadili.

Kuna kitu si bure. Ndani ya jeshi la Polisi kuna kitu hakipo sawa
Kifo cha Polisi wewe kinakuuma?!!
 
Nilishawahi kuingia selo mara mbili na askari
wanavua kila kitu yani mkanda na viatu na wanajichanganya na mahabusu wengine

Labda huyo koplo walimpeleka selo ya peke yake na wakampa vifaa vya kujitundika!
 
Sorry to say,
Ila mi naonaga police majority watu fulani wasioweza kbs kufanya vitu kwa weredi, mission zao zimekaq kijinga jinga kama watu wasio watalaam katika eneo hilo.

Anyway nina maswali yangu kwa
RPC, IGP na Waziri wa Mambo ya ndani;
1. Alijinyonga kwa kutumia kitu gani, na kiko wapi kama ushahidi?

2. Kama mahabusu walikuwa watu sita, kwa nini hakuna aliyegundua mapema?

3. Kama kuna CCTV za kituo zinaonyesha nini kabla na wakati wa tukio?

4. Nani alikuwa na ufunguo na access ya chumba cha mahabusu?

5. Forensic imewezaje kuthibitisha kuwa ni kujinyonga na si kunyongwa?

6. Post-mortem imebaini majeraha gani mengine mwilini?

7. Je, mwili ulifanyiwa toxicology ili kujua kama alikuwa ametumia dawa/sumu au kitu kingine?

8. Kwa nini taarifa ya kifo imechelewa kutolewa, licha ya tukio kutokea tarehe 27 Agosti?

9. Kwa nini uchunguzi wa kifo unafanywa na mfumo huo huo uliokuwa unamshikilia marehemu na ambao ndani yake wapo watyhumiwa wengine?

10. Je, Serikali iko tayari kwa uvhunguzi huru ukihusisha kuchunguzwa kwa OCD, OC CID, RPC, IGP na Waziri wako tayari kwa uchunguzi huru wa forensic na kuweka matokeo wazi?

Assumptions 5 za Kuchunguzwa
Custody failure:

1. Je, taratibu za ulinzi wa mahabusu zilikiukwa kwa mujibu wa PGO?

2 Scene contamination: Nani aliingia eneo la tukio wa kwanza?

3. Cause of death: Je, ushahidi wote unaendana na kujinyonga?

4. Evidence integrity: CCTV, nguo, ligature na samples zilihifadhiwa vizuri, kama haukuhifadhiwa vzr kwa nn nani anawajibika?

5. Unexplained injuries: Kucha, macho au majeraha mengine ni kweli yapo, na yalisababishwa na nini?

Kesi hii haihitaji hitimisho la haraka; inahitaji ushahidi unaoweza kuthibitishwa.
 

Attachments

  • 1000020485.jpg
    1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 8
Kufuatia kifo cha askari huyo, uchunguzi wa kisayansi uliofanyika na ndugu zake kushuhudia ulibaini chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga.
Nani alimpa facilities za kujinyongea ikiwa ni pamoja na sehemu ya kujitundika
 
Hakuna haja ya wananchi kutoa hukumu kabla ya uchunguzi kukamilika. Lakini kwa upande mwingine, hakuna haja pia ya wananchi kunyamazishwa kwa kuambiwa kila swali ni upotoshaji. Tukio limetokea akiwa chini ya ulinzi wa mamlaka, hivyo ni halali kuuliza maswali kuhusu mazingira ya kifo. Kinachotakiwa ni uchunguzi wa wazi, wa kitaalamu na unaoweza kujenga imani kwa umma.
Mtuhumiwa wa hicho kifo ni nani na anayefanya uchunguzi ni nani?
 
View attachment 3660766
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linapenda kutoa taarifa kuhusu kifo cha askari namba. H.1796 Koplo Mwita, aliyekuwa akishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi katika kituo cha Polisi Wilaya ya Tanga.

Tarehe 27 Agosti 2026 majira ya saa moja na dakika tatu usiku, askari huyo alikutwa akiwa amefariki dunia ndani ya chumba cha mahabusu katika kituo hicho

Kabla ya kifo chake, marehemu, pamoja na Afisa mmoja na Askari watano wa Jeshi la Polisi wa vyeo mbalimbali, walikuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kijinai.

Kufuatia kifo cha askari huyo, uchunguzi wa kisayansi uliofanyika na ndugu zake kushuhudia ulibaini chanzo cha kifo chake ni kukosa hewa kutokana na kujinyonga.

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya taratibu za mazishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linatoa rai kwa baadhi ya Wananchi,baadhi ya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuandaa na kusambaza taarifa zisizothibitishwa au kutoa hitimisho lisilotokana na matokeo rasmi ya kiuchunguzi, kwani kwa kufanya hivyo ni upotoshaji ambao ni kinyume cha sheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kuwa uchunguzi wa tukio hili unaendelea kukamilishwa kwa kuzingatia taratibu zote za kiuchunguzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Imetolewa na

Kamanda wa Polisi. Mkoa wa Tanga

MY TAKE

Polisi anawezaje kujinyonga Mahabusu huku kukiwa na watu wengine watano?

Wanadai uchunguzi umebaini alikosa hewa. Kwanini hakukosa hewa kabla ya kutuhumiwa hayo makosa ya Jinai?

Je, ni nani alimn'goa kucha na kumtoboa macho?

Ukweli utajulikana na sisi tutazidi piga kelele.

Kumbuka kifo kilitokea 27/08.2027 jioni wakauchuna kutoa taarifa wakijua litapita. Baada ya watu kupiga kelele ndo tarehe 31/08/2026 jioni wametoa taarifa huku wakikataza watu kujadili.

Kuna kitu si bure. Ndani ya jeshi la Polisi kuna kitu hakipo sawa

Halafu kwenye barua wametaja jina moja tu ili watu wasie nani ni nani. Mtaani anajulikana kama Afande Mecky kwani jina lake ni Mwita Mecky Milumbe. Kwanini wanamtaja kwa kuibia?
View attachment 3660837
Hakuna pole kwa familia wala majonzi!
 
Back
Top Bottom