Polisi Tanzania wamtaka Mwamposa kujisalimisha

MUNGU anaishi ndani mwetu ,hakuna kiranja wala mtu aliyetumwa hapa duniani kukutanisha na MUNGU ,tenda mema fuata maandiko yake na amri zake hakika utayashuhudia mema yake hao wanajifanya mitume wanawaibia pesa zenu tangu enzi za mtume muhamadi na yesu kristo MUNGU hajawahi kutuma kiumbe huku duniani namalizia hakuna KIRANJA wala balozi wa kukutanisha na MUNGU yupo ndano ya mioyo yetu



Jumapili njema,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kwenda pale Kawe na watoto wangu kukanyaga mafuta mwee mwee yaani vurugu msukumano watoto wanaliaa mpaka nilijuta.

Namuombea hili suala liishe, siwezi muhukumu kwa lolote maana hata mimi nina madhambi yangu
 
Kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madkta Tunaambiwa ni zaidi ya 30

*Bull dozer
*Cheni yenye nyoka
*Kumwaga mafuta mlangoni
*Muda wa usiku
* Wanawake ndio wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya 16 waliokufa 15 ni ke .....yaani wanawake bwana wanawaheshimu wachungaji kuliko waume zao,,,,akili zao wanazijua wenyewe.

Rest in peace marehemu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wa hayati Mwalimu Nyerere, ahkukuwa na upumbavu huu.
Mwalimu Nyerere alisema.
" Serikali haina dini ila watu wake wana dini"
" Inchi inaweza kupata kiongozi ambaye hana dini lakini lazima tutafute namna ya kumwapisha"
Wakati wa Mzee Mwinyi, Inchi iliingia katika malumbano ya Kidini ambako kila dini ilikuwa inashambulia dini ingine hasa Wakristo na Waislamu.
Wakati wa Mkapa malumbano ya Kidini yalifutiliwa mbali na kukaanza manabii wa uongo ambao kila moja alianzisha kanisa lake.
Hadi sasa kuna amani kubwa na heshima kati ya Wakristo na Waislamu ila kumejitokesa manabii wengi wa uongo ambao wamegeuza Ukristo kama biashara kwa kuiunganisha na mazingaombwe ya kishirikina.
Serikali ichukue hatua kwa kuyatoza kodi makanisa yote yanayomilikiwa na watu binafsi badala ya taasisi zenye muundo wa kumilikiwa na waumini.
Klabu ya mpira kama ya Simba inajipeleka kumilikiwa na mtu binafsi kama haya makanisa na baadaye mhusika atakuwa ananufaika kibiashara bila kulipa kodi na wanachama kubaki washabiki wa kushangilia tu Simba ikishinda. Mwenye Simba atashangilia mapato zaidi kuliko ushindi na muda wowote anaweza akaiuza kwa mtu yeyote hata mshabiki wa Yanga ili mradi apate pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…