google helper
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 9,667
- 13,876
Mikutano inayojumuisha Idadi kubwa hivi ya watu hivi polisi huwa hawashirikikuangalia Usalama? Pamoja na Yaliyotokea Polisi nao hawakutekeleza Wajibu wao
Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Hata mtini kuna kazi ya kuukwea mti wao wanataka wapewe mdomoniBaraka za miteremko haziwez kukufikisha popote
Kuna mitume walipigwa mawe & kuchomwa moto ndio wakaiona mbingu, we utoke na ujinga wako ukachukue baraka kama tunda mtini
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha anaogopa utume wa virungu vya polisi na gerezan kama kwa pauloNabii anatowekaje ???
Mtume wa Mungu anakimbia polisi ?????
Mbona akina Paulo walikuwa wanakaa gerezani ?? Akina Petro walifungwa Sana tuu inakuwaje huyu anakimbia ???
Sent using Jamii Forums mobile app
Mara mwakajinga, mwapumbavu, mwaupuuzi nkDuh hivi hawa wanyakyusa wenzangu hawana uwekezaji mwingine zaidi ya dini,dah mara Mwamposa mara Mwambapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya Hamida kuongeza dawaWanawake mna nini, maana ndio mmejaa huko kwa Hawa matapeli.
Reli na kichekesho kitakuwa cha kwakokwa hiyo tubonyeze nyota au reli ili kupata kichekesho?
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limemtaka mtume Boniface Mwamposa kujisalimisha mwenyewe polisi kwa mahojiano kutokana na vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro jana usiku Jumamosi Februari Mosi, 2020.
Watu hao walifariki usiku wakati waliposhiriki kongamano la kidini uwanja wa Majengo, wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyomwagwa milango ya kutokea uwanjani.
Wakati Jeshi hilo likimsaka kwa udi na uvumba kiongozi huyo wa kiroho, Jeshi hilo linawashikilia watu saba akiwamo mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa kwa mahojiano.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 2, 2020 amesema mchungaji huyo ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi.
“Baada ya hilo tukio tumemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa ambaye ni maarufu kwa jina la Bulldozer bila mafanikio. Kupitia kwenu tunamtaka ajisalimishe kwa mahojiano,” amesema
Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, wawili wakiwa ni wa kike na watu wazima 16 wakiwamo wanawake 15.
Kwa mujibu wa Kamanda Hamduni, katika tukio hilo watu waliojeruhiwa ni 16 na wawili kati yao hali zao sio nzuri na kwamba kazi itakayoendelea kuanzia asubuhi ni kutambua miili ya marehemu iliyohifadhiwa Hospitali ya Mawenzi.
Mwananchi
Daah nimeandika nimefuta [emoji856]Nilishawahi kwenda pale Kawe na watoto wangu kukanyaga mafuta mwee mwee yaani vurugu msukumano watoto wanaliaa mpaka nilijuta.
Namuombea hili suala liishe, siwezi muhukumu kwa lolote maana hata mimi nina madhambi yangu
Kweli kabisa na najitahidi mnoo kuweka ulinzi wa watu kupunguza vurugu ila sisi binadamu tu akili zetu utadhani yanaisha kumbe walaaaa hayaishiNilishawahi kwenda pale Kawe na watoto wangu kukanyaga mafuta mwee mwee yaani vurugu msukumano watoto wanaliaa mpaka nilijuta.
Namuombea hili suala liishe, siwezi muhukumu kwa lolote maana hata mimi nina madhambi yangu
Usichukulie serious kila kitu mkuu.Waliouawa ni wanyakyusa?. Kilimanjaro waliokuwa wanagombea upako ni wanyakyusa? Una-fail wapi wewe?. Mnyakyusa Mwamposa yeye ana shida na hela za hao wenzio waliokuwa wanagombea upako
Sent using Jamii Forums mobile app
Kumwelekeza Mpumbavu ninkazi ngumu ,, pole sana mana mtu hajawah vuka hata mkoa atakuelewajeKukariri kunakotokana na elimu ya kukariri! Moshi hawaishi wachaga tu.
Kingereza unajua wewe tu uliezaliwa uingereza. Umejuaje nimechukia?Usichukulie serious kila kitu mkuu.
Na uzuri nimeandika kabisa kwamba hiyo ni joke.
Hujui kiingereza au huwa unachukia mpaka utani?
Sent using Jamii Forums mobile app