DOKEZO Polisi Trafiki wa Arusha mnakera sana kuwasimamisha watembeza watalii bila sababu, mkikosa kosa mnaomba rushwa

DOKEZO Polisi Trafiki wa Arusha mnakera sana kuwasimamisha watembeza watalii bila sababu, mkikosa kosa mnaomba rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mawele

Senior Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
119
Reaction score
320
Habari.

Mimi ni Safari Guide, nina Kero kubwa sana kuhusu Traffic Police wa Arusha.

Wamekuwa wakisimamisha magari ya watalii kila mahali hawajali kama umebeba wageni au la, waanza kuomba leseni na kukagua gari wanachukua hadi dakika 10 wamekusimamisha bila kujali umetoka wapi na unaratiba gani na wageni.

Kikubwa siyo ukaguzi ni rushwa tu wanataka wanakwambia wewe una hela sisi tupo njiani tumepigwa na jua “fanya mpango” hii kero ni kubwa sana na wanahakikisha wamevaa koti na kufunika majina yao wakiogopa kurekodiwa.

Mfano juzi tarehe 24, walinisimamisha, yule trafiki akamwomba mwenzake koti kisha mwenzake akasogea mbali ili tusione namba yake alitumia dakika 5 kuniuliza maswali yasiyo na msingi pia hayakuhusu hata usalama wa barabarani alinza umetoka wapi? Hawa wageni wa nchi gani? Ulikuwa safari siku ngapi? Ujaoa mzungu wewe?

Aisee kile kitendo wageni hawakufurahishwa nacho wakadai kuandika sifa mbaya kwa traffic wa Tanzania niliongea nao na kuwaeleza kuwa hakuwa na nia mbaya wakaelewa muda mwingine unakuwa umechelewa au wageni wamechelewa kutoka hotelini na mnawahi ndege basi askari anaanza kukupotezea muda ukimkomalia kuwa akuachilie uondoke anakwambia ana baki na leseni yako ukitoka KIA umpigie simu umtoe ndo akupe anakwambia andika namba zangu.

Maoni: Kuna Police Tourism ilianzishwa ni kama vile imekufa wapo tu wanangojea vikesi vya utalii wa vifanye mtaji, ila ni vyema zitumike kumaliza kero hii, kama inafaa driver guide apewe hati ya ukaguzi siku moja kabla ya safari au apite kwa ofisi za hao Police Tourism akatiwe kibali anapokuwa anakwenda safari ili kuepusha hizi kero, wamiliki wa biashara ya utalii wanatumia nguvu kubwa sana kuwapata hawa wageni ni vyema chombo husika kusimamia hilo.
 
Aisee Poleni Sana Ila hii kantri sijui nani alituloga Mpaka tumekua Hivi yani kila sehem kero dhuruma, rushwa, wizi Yani kilak2
 
Toa pesa fanisha jambo lako
Tanzania hakuna haki
Unashindwa nini kumpa traffic buk 2 ukatembea na wateja wako
 
Kwahiyo ulitakaje 🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓 kusema usingebeba wageni je ?
""" Wamekuwa wakisimamisha magari ya watalii kila mahali hawajali kama umebeba wageni au la"""
 
Back
Top Bottom