Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Tarehe 16 Novemba 2024 eneo la Kariakoo Dar es salaam kulitokea tukio la kuporomoka kwa jengo la biashara. Wakai jitihada mbalimbali zikifanywa na Serikali na sekta binafsi kuhusiana na jinsi ya kuwaokoa watu katika eneo hilo , zilipatikana taarifa za watu wasio na mamlaka yoyote ya kisheria ya kushughulikia majanga yenye sura ya kitaifa , kuanza kukusanya pesa kwa kutumia akaunti zao binafsi suala ambalo ni kinyume na Sheria na Kanuni zinazoshughulikia majanga.
Watuhumiwa wawili wamekamatwa na wanahojiwa kwa kina. Waliokamatwa ni Diva Gissele Malinzi miaka 36, mkazi wa Mikocheni amekamatwa Dar es Salaam na Jenifer Jovin Bilikwija miaka 25, mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam litashirikiana na Mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hawa.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au watu ambao yanapotokea matatizo au majanga wao huona ni fursa ya kujinufaisha.
Pia soma:

- Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
- Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa