Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni banana state wanaowashikilia watuhumiwa kabla ya upel3lezi kukamilika.Tarehe 16 Novemba 2024 eneo la Kariakoo Dar es salaam kulitokea tukio la kuporomoka kwa jengo la biashara. Wakai jitihada mbalimbali zikifanywa na Serikali na sekta binafsi kuhusiana na jinsi ya kuwaokoa watu katika eneo hilo , zilipatikana taarifa za watu wasio na mamlaka yoyote ya kisheria ya kushughulikia majanga yenye sura ya kitaifa , kuanza kukusanya pesa kwa kutumia akaunti zao binafsi suala ambalo ni kinyume na Sheria na Kanuni zinazoshughulikia majanga.
Watuhumiwa wawili wamekamatwa na wanahojiwa kwa kina. Waliokamatwa ni Diva Gissele Malinzi miaka 36, mkazi wa Mikocheni amekamatwa Dar es Salaam na Jenifer Jovin Bilikwija miaka 25, mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam litashirikiana na Mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hawa.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au watu ambao yanapotokea matatizo au majanga wao huona ni fursa ya kujinufaisha.
Pia soma:
- Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
- Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa
Kabint kanaonekana kajinga vile hiyo akili atatoa wapi.Kama niffer aisee akisema miamala flani ni ya mzigo ataulizwa efd risiti yake
Kama hakutoa fine ya kutotoa risiti.
Wanasema na account nzima yaani
Bora angesajili namba mpya
Huna Akili....A good Police Officer is only a dead Police Officer.
Jeshi la Polisi badala ya kuwakamata Watu waliohusika katika kusababisha ajali na kisha kuwafikisha Mahakamani wao wanahangaika na Watu waliokusanya michango ya maafa.
Yaani hovyo kabisa.
Unadhani hawajakamatwa?A good Police Officer is only a dead Police Officer.
Jeshi la Polisi badala ya kuwakamata Watu waliohusika katika kusababisha ajali na kisha kuwafikisha Mahakamani wao wanahangaika na Watu waliokusanya michango ya maafa.
Yaani hovyo kabisa.
Msamaria mwema au tapeli tu. Si angetoa mchango wake ye mwenyewe, si ana maduka kibao. Alaf hata kwny hilo tukio hajafika, mtu yupo dodoma anafurahi kufungua duka lake, eti anachangisha. Asee watz sijui ujinga utawaisha lini.Binti mdogo wa miaka 25 ana trend kwa kuchangisha michango ya maafa, huyu si ndio angepongezwa kwa kufanya hivyo chapchapu wakati mamlaka husika imelala? cha ajabu ananakamatwa. itungwe sheria ya msamaria mwema
Wajinga ndio waliwao.Wivu kama wivu mwingine
Mimi binafsi siwezi kushawishika kuchangia mfuko wa serikali ila nimechangia pesa kwa nifer
Sababu. Namuamini
Kila mtu ana mawazo yake na uhuru na utashi wa kutoa maoni watu wengi Imani ya kifedha hatuna na watu wa huko tunawaamini Hawa watu wa mtaani
Kuna wana flan nipo nao job, yan hawa jamaa tokea lile tukio la kariakoo litokee cjawah kuwaskia wakizungumzia kwny mazungumzo yao. Yani kila mda ni mipira tu. Mpk nikajisemea tu kwel hii nchi acha watawala waeendelee kutuburuza, maana wananchi wengi bado ni wajinga sana.CCM izuie mjadala iwe iweje? Katika nchi ambayo uongozi wa nchi hauna pressure ya kuogopa mijadala ya wananchi basi ni Bongo. Wananchi wenyewe siku mbili tu wanakuwa wameshasahau kila kitu. N kama majoka ya kibisa tu, hawana madhara.
Watuhumiwa wa kwanza na muhimu kabisa hawajahojiwa.Vipi wazembe waliosababisha hii dhahama ya Jengo kudondoka wameshakamatwa na Kuhojiwa ?
ni mtangazaji wa redio huko dar, kwani we humjui diva?Diva ndo nani huko Darisalama?