Polisi: Tunawashikilia Niffer na Diva kwa mahojiano na hatua nyingine za Kisheria

Polisi: Tunawashikilia Niffer na Diva kwa mahojiano na hatua nyingine za Kisheria

Tena huyo Diva ndio tapeli kabisa, bora hata Niffer tunaweza kumpa the benefit of doubt.

Diva kodi ya nyumba tu mpaka akamlilie Diamond, ndio awafikishie michango yao wahanga wa K/Koo? Teh
Kumbe wanajulikana si waaminifu?
 
Okay hii inaitwa enjoy my city view while u can , cauz u crack my City rule tehehehe.
Mambo ya I dont mean to disrespect officer hayana nafasi
 
Pressure ya kariakoo ilikuwa kubwa sana, atleast mmepata pa kupumulia. Wataalam tunaiita propaganda.

Kitendo cha serikali au taasisi kutumia tukio jingine ili kuhamisha au kupunguza umakini wa umma kutoka kwenye tukio linalowahusu hujulikana kitaalamu kama "distraction" au "agenda setting manipulation". Kwa lugha nyingine, inaweza pia kuitwa:

1. "Diversionary Tactic": Mbinu ya kupotosha au kuhamisha umakini wa umma kutoka kwenye suala nyeti.
2. "Smoke Screen": Njia ya kuficha ukweli kwa kuleta mada nyingine ya kuvutia au yenye mjadala mkali.
3. "News Drowning": Mbinu ya kuzidisha habari nyingine ili kufunika habari nyeti.

Hii ni sehemu ya mbinu za propaganda au public relations spin, zinazolenga kudhibiti maoni ya umma na kuzuia mijadala kuhusu suala fulani.
Yes, Spinning Propaganda Tactics.
 
Binti mdogo wa miaka 25 ana trend kwa kuchangisha michango ya maafa, huyu si ndio angepongezwa kwa kufanya hivyo chapchapu wakati mamlaka husika imelala? cha ajabu ananakamatwa. itungwe sheria ya msamaria mwema
Yule binti nilmshangaa.
Waziri Mkuu anatoa taarifa kuwa akamatwe, yeye anashangilia kuwa hata Waziri Mkuu kamtambua na anajua yupo.
Haijui Serikali huyu na makali yake!
 
Tena huyo Diva ndio tapeli kabisa, bora hata Niffer tunaweza kumpa the benefit of doubt.

Diva kodi ya nyumba tu mpaka akamlilie Diamond, ndio awafikishie michango yao wahanga wa K/Koo? Teh
Nilikuwa nina hofu kubwa baada ya kuona hilo jina la Nifah! Ahueni sasa nimepata amani baada tu ya kuona hii comment yako hapa!😇
 
Roho
Ni kweli ni mdogo ila hicho kiherehere chake ndio hunifanya nisimkubali pia.
Roho iliniruka kwa huzuni Jana nilipoona hilo jina ni wewe ,nikawaza vipi yule shemeji atajisikiaje ila nilipoona umejibu nilifarijika .

Keep hustling dada ,pamoja ,ana kihehere Sana huyo dada ila akitoka aje kwanza ajibu kwa hili jina la bilikwija nina mengi ya kumuuliza
 
Celebrity Uchwara wa bongo walishapata kichaka cha kupiga hela!
Kama mna hela toeni tu, hakuna ujasiri wowote kwenye kuchangisha! Shenzy zenu!
Uko sahihi kabisa. Huu ni mchongo na walishaona sehemu ya kupiga fedha. Dunia ya sasa haina watu wema kiasi hicho hasa hawa celebrity uchwara. Walikuwa wanatafuta fedha za kufanya surgeries za kuongeza urembo
 
Tarehe 16 Novemba 2024 eneo la Kariakoo Dar es salaam kulitokea tukio la kuporomoka kwa jengo la biashara. Wakai jitihada mbalimbali zikifanywa na Serikali na sekta binafsi kuhusiana na jinsi ya kuwaokoa watu katika eneo hilo , zilipatikana taarifa za watu wasio na mamlaka yoyote ya kisheria ya kushughulikia majanga yenye sura ya kitaifa , kuanza kukusanya pesa kwa kutumia akaunti zao binafsi suala ambalo ni kinyume na Sheria na Kanuni zinazoshughulikia majanga.

Watuhumiwa wawili wamekamatwa na wanahojiwa kwa kina. Waliokamatwa ni Diva Gissele Malinzi miaka 36, mkazi wa Mikocheni amekamatwa Dar es Salaam na Jenifer Jovin Bilikwija miaka 25, mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar es salaam.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam litashirikiana na Mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hawa.

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au watu ambao yanapotokea matatizo au majanga wao huona ni fursa ya kujinufaisha.

Pia soma:

Wapelekwe mahakamani kama wamekosea.
 
Tena huyo Diva ndio tapeli kabisa, bora hata Niffer tunaweza kumpa the benefit of doubt.

Diva kodi ya nyumba tu mpaka akamlilie Diamond, ndio awafikishie michango yao wahanga wa K/Koo? Teh
Fedha haina cha huyu ni afadhali. Narudia, fedha haina cha huyu ni afadhali. Tafuta notebook uandike hiyo sentensi, itakusaidia baadae.
 
Nguvu iliyotumika kwa niffer mngetumia kwa wezi wa serikalini au vigogo
Watanzania tungeishi kama Bruney
Pam kazingua
Katumia zaidi mihemko na kiki ili wazidi kuzima presha za watu kutaka kujua mmiliki na injinia wa lile jengo
Mungu atamlipa nifer kwa nia yake ya dhati
 
Pressure ya kariakoo ilikuwa kubwa sana, atleast mmepata pa kupumulia. Wataalam tunaiita propaganda.

Kitendo cha serikali au taasisi kutumia tukio jingine ili kuhamisha au kupunguza umakini wa umma kutoka kwenye tukio linalowahusu hujulikana kitaalamu kama "distraction" au "agenda setting manipulation". Kwa lugha nyingine, inaweza pia kuitwa:

1. "Diversionary Tactic": Mbinu ya kupotosha au kuhamisha umakini wa umma kutoka kwenye suala nyeti.
2. "Smoke Screen": Njia ya kuficha ukweli kwa kuleta mada nyingine ya kuvutia au yenye mjadala mkali.
3. "News Drowning": Mbinu ya kuzidisha habari nyingine ili kufunika habari nyeti.

Hii ni sehemu ya mbinu za propaganda au public relations spin, zinazolenga kudhibiti maoni ya umma na kuzuia mijadala kuhusu suala fulani.
CCM izuie mjadala iwe iweje? Katika nchi ambayo uongozi wa nchi hauna pressure ya kuogopa mijadala ya wananchi basi ni Bongo. Wananchi wenyewe siku mbili tu wanakuwa wameshasahau kila kitu. N kama majoka ya kibisa tu, hawana madhara.
 
Hawa wanaojiona maarufu watafute njia nyingine za kudumisha huo umaarufu wao mambo mengine ni kujitafutia matatizo na kujitia aibu ya bure kwa kuonekana ni matapeli.
Mtu wewe unajua siyo muhusika kiherehere cha nini?
 
Back
Top Bottom