A good Police Officer is only a dead Police Officer.
Jeshi la Polisi badala ya kuwakamata Watu waliohusika katika kusababisha ajali na kisha kuwafikisha Mahakamani wao wanahangaika na Watu waliokusanya michango ya maafa.
Yaani hovyo kabisa.
Huna Akili....
…....….................
...........................
Napenda kutoa ushauri ufuatao kwa watu wenye ushawishi kwa jamii;
1. Kukitokea maafa/janga la kitaifa, usichangishe fedha. Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2022, kifungu cha 26(2) inasema jukumu la kuchangisha litafanywa na Kamati ya maafa iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu, kupitia akaunti maalumu.
2. Ukichangisha fedha kwa matatizo mengine ambayo si maafa (eg matibabu, elimu, yatima) usitumie namba/akaunti binafsi. Ni kosa kisheria. Tumia taasisi (NGO) iliyosajiliwa.
Kwa mujibu wa Sheria ya NGO namba 24 ya mwaka 2002, kifungu cha 32, michango ya kibinadamu (charitable initiatives) inaratibiwa na mashirika yaliyosajiliwa na sio mtu binafsi. Lengo la sheria ni kuweka "Check & Balance" ili kudhibiti ubadhirifu kwa sababu NGO inafanyiwa auditing angalau mara 2 kwa mwaka (internal & external).
3. Kama unataka kumsaidia mtu na huna NGO, tumia namba za mhusika mwenyewe, lakini kwanza upate kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya. Kifungu cha 122 cha sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inataka michango inayokusanywa na mtu binafsi kwa ajili ya "charity" ipate kibali kwa DC.
#Swali: Je watu wanafahamu haya?
#Jibu: Hapana. Kuna watu wanachangisha pesa kwa nia njema kabisa (utmost good faith) lakini hawajui utaratibu wa kisheria ulivyo.
#Swali: Je nini kifanyike?
#Jibu: Wapewe elimu. Hawapaswi kutishwa, kubezwa au kukatishwa tamaa. Kama mtu amechangisha fedha kupitia akaunti yake binafsi ili aokoe maisha ya mgonjwa kwanini umshtaki? Ni kweli hajafuata utaratibu lakini kafanya jambo jema. Kwahiyo kunaweza kuwa na "actus reus" lakini kusiwe na "mens rea" na hivyo ikawa ngumu kuestablish jinai.
#Points3ZaKukariri;
1. Michango ya maafa/majanga inakusanywa na serikali tu.
2. Michango ya "charity" inakusanywa na taasisi/NGO iliyosajiliwa na inayowasilisha auditing report wizarani.
3. Ukitaka kuchangisha na huna NGO tumia namba/akauti za mhitaji mwenyewe kwa kibali cha DC.
#UshauriKwaSerikali: Watanzania wanapendana sana, lakini wengi hawana imani na serikali kuhusu michango. Wanakumbuka kuchangia wahanga Kagera pesa zikabadilishwa matumizi. Kwahiyo tumieni watu wenye ushawishi kuhamasisha (eg wasanii, viongozi wa dini, wanamichezo, wanahabari etc).!
Credit.... Malisa GJ. Facebook.