Mkuu wa kikosi cha Polisi cha Usalama wa barabarani ACP Ramadhani Ngazi asema kuna changamoto za kiusalama. Ni kwenye baadhi ya mikoa kutokana na ujambazi n.k Akitaja maeneo ya Rukwa, Katavi, Kagera kuna mapori ambayo ni tishio kwa utekaji.
Akizungumza mbele ya kikao cha LATRA baada ya azimio la bunge kupitia hoja ya spika wa Bunge kuwa mabasi yasafiri usiku.
Pia wadau waomba mabasi ya safari ndefu kuwa na madereva zaidi ya mmoja ambao watapokezana kuendesha mabasi ili kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na uchovu unaosababisha madereva kutokuwa makini.