Bwana Tony Cipriano
JF-Expert Member
- Nov 17, 2022
- 4,401
- 9,555
Mimi binafsi sina imani tena na jeshi la polisi.
Siyo tu kosa, hukumu yake ni kumiminiwa risasi zisizohesabika, na kufukiwa juu chini, hivi ni kweli ndipo tulipofikia? Au naota tu?Basi kwa hapo kosa ni uhaini. Wameshapata kosa la kuwapa watu siku hizi. Tuko kwenye wakati mgumu sana sana. Sijui tunatokaje hapa. Sheria hazifuatwi. Kuandamana na kuhamasisha maandamano ni kosa kikatiba.
Kwani maandamano tangu lini ni makosa ya jinai? Ninyi polisi mnatushangaza sana.Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linapenda kutoa ufafanuzi juu ya picha mjengoe zinazoonekana katika baadhi ya mitandao ya kijamii zikieleza kuwa, kuna vijana wawili wametekwa Jijini Arusha.
Taarifa sahihi ni kwamba, kwa nyakati tofauti tuliwakamata na tunaendelea kuwahoji vijana hao ambao ni Edwin Richard Mboro (29) mkazi wa Sanawari Jijini Arusha na Victor Bonaventure Ndibalema (35) mkazi wa Kijenge kutokana na tuhuma za kupanga na kuhamasisha Maandamano kinyume cha Sheria.
Uchunguzi wa tukio hili unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe.
Pia Soma: Video: Kijana akitekwa na watu wenye silaha nzito Arusha