Mkumbushe pia kua wanawake wengine wapo fit 💪
Nb siungi mkono mauwaji
Mimi sipingi kuwa mwanamke hawezi kumuua mwanaume.
Aina ya kifo cha Nyanza kilivyotokea kunaonyesha kuna pattern ya matukio mengi ambayo ukiunga dots ni ngumu kusema haya mauaji yamefanywa na mtu mmoja pasipo ushiriki wa mtu mwingine.
Mwanamke anaweza kukuua kwa sumu, kukuua hata kwa panga kama umelala nk. Hayo yote nakubali.
Nimeweka benefit of doubt kwa kuonyesha uwezekano wa mwanamke kuweza kutekeleza hayo mauaji peke yake, lakini pattern ya matukio yanaongeza maswali ambayo yanafanya iwe ngumu kuamini kuwa haya mauaji yamefanywa na mtu mmoja tena mwanamke.
Mwili umepatikana ukiwa unaonyesha majeraha makubwa eneo la kichwa, concept ya kwanza ni kwamba alishambuliwa kichwani.
Anza kui analyze hiyo concept kwa kuitengenezea picha ndio hapo utaona hoja yangu. Kwamba wakati Nyanza anashambuliwa alikuwa katika hali gani?
1. Je wakati anashambuliwa alikuwa hajitambui (unconcious) chochote eidha alilala?
2. Au alikuwa anaona shambulio linavyokuja ila hakuji defend?
3. Au shambulio aliliona likija ila alikuwa amefungwa kamba hakuweza kujitetea?
4. Na kama 3 ni kweli je mwanamke mmoja anatosha kumfunga kamba mwanaume ambaye ana concious?
5. Baada ya mauaji ulitumika usafiri gani kubebea mwili mpaka kuuleta Chanika kwa ajili ya kuufukia?
6. Sina hakika na huyo mwanamke kumiliki gari ila mashaka yangu kwa info zake nilizopata japo kwa uchache, hana maisha hayo, sasa ina maan alibeba maiti mgongoni kutoka Kigamboni hadi Chanika?
7. Kama 6 haiwezekani basi ni wazi kulikuwa na usafiri, je huyo mwenye huo usafiri alikuwa hajui kilichokuwa kinabebwa?
Maswali ni mengi.