Ulaya mtu anazikwa sebuleni na ndugu mnakaa humo humo ndani mkipiga story hadi siku muuaji awaambie hapa nilimzika fulani.hata hivyo wanawake wa Tanzania 50/50 wanaifanya kwa vitendo,mwanamke kuua mtu kumburuza hadi nyuma ya nyumba kisha kumfukia siyo kazi rahisi wapewe mauwa yao.
Hapa umenikumbusha kuna documentary moja niliiangalia inaitwa The secrets We Bury (2025), kwenye hii documentary inasimulia simulizi ya mtu ambae alikua Mwanajeshi wa Marekani ambae alifariki kifo cha kutatanisha yaan alipotea tu ghafla na hakuwahi kuonekana tena, basi kipindi anafariki watoto wake walikua ni wadogo sana ingawa dada yao mkubwa ndie aliekua mkubwa kidogo, basi kisa kipo hivi Baba yao kuna siku alirudi na Mgeni nyumbani kwao Mgeni ni Mwanaume sasa aliporudi nae akawa anasaidiana nae kufanya marekebisho ya nyumba, nifupishe kwenye hizo harakati za ujenzi huyo Baba yao ndipo alipopotea na hakuonekana tena,
Mama yao akaolewa na yule Mgeni alieletwa na Baba yao wakaendelea kuishi, sasa walipokua wakubwa Mama yao akawa anataka kuiuza ile nyumba yao, mtoto wa Mwisho wa Kiume akamwambia hapana Mama usiiuze hii nyumba mimi nitainunua kweli akainunua ile nyumba akaanza kuishi na Mama yake ndio taratibu za wazungu, Mama yao baada ya kutengana na huyo Mgeni ndio akataka aiuze nyumba yao, mtoto akainunua akaendelea kuishi na Mama yake
Sasa huyu mtoto wa Mwisho wa Kiume akaanza taratibu za kumtafuta Baba yake yaan hata km amekufa popote basi wayapate tu hata mabaki yake tu akawa anakusanya mabaki mbalimbali na taarifa mbalimbali kwenye majalala ya takataka, madampo yaan akawa km hawa watu wanaokota makopo huku bongo yeye anachomba taarifa yaan ili km atakutana na taarifa yoyote inayolink na Baba yake ila ni mtu mwenye nyadhifa kubwa maana alisomea udaktari na ni daktari wa binadamu,
Akaendelea kutafuta kila akimuuliza Mama yake hampi majibu ya kueleweka kumbuka huyu mdogo kipindi anamtafuta Baba yake yeye tayari kashazeeka na ana watoto tayari na wenyewe ni wakubwa na wana watoto ila yeye alikua anatafuta mabaki ya Baba yake, akaendelea kutafuta, kufupisha kidogo baada ya kifo cha Mama yake dada yake akamwambia na yeye anaungana nae kumtafuta Baba yake ila atampeleka kwa mtu anaefanya masuala ya Psychic 🔮
Kwanza jamaa anasema yeye alikua haaamini kabisa hayo masuala ya Psychic ila kwa heshima ya dada yake na kutokumkatisha tamaa dada yake akakubari wakaenda ingawa ndugu zake wengine waligoma hilo suala la kwenda huyo mtu wa Psychic, basi walipoenda yule Mama anaefanya masuala Psychic akaanza kuwaelezea masuala mengine kabisa jamaa akaona km vile anawapotezea muda tu, akawa km anataka kumpuuza aondoke maana aliona km anapoteza muda yule Mama akamwambia ulikua unataka nikwambie kuhusu nini unachokihitaji sana, akamwambia mimi nataka nijue yalipo mabaki ya Baba yangu, yule Mama bila kupepesa macho akamwambia kwenye nyumba yenu
ndani ya Chumba cha kulenga shabaha chini pale usawa wa ile board ya kulengea shabaha ndipo alipozikwa Baba yenu amezikwa pale, kumbuka Baba yao alikua Mwanajeshi wa Marekani.
Dada yake hakua anapafahamu ila yeye alipafahamu sababu mara nyingi Baba yake alikua anamchukua wanaenda pale anaanza kulenga shabaha na yeye anakua anamuangalia
Ndipo wakarudi yule Mzee akachukuana na wanawe wawili mapacha wakaanza kuchimba pale alipoelekezwa na yule Mama anaefanya masuala ya Psychic, wakachimba lakini hawakufanikiwa kupata kitu, basi Mzee akawa km amekata tamaa kwamba amemkosa kumpata Baba yake, lakini wale wanawe mapacha wakasema Mzee pumzika sisi tutajitahidi kutafuta km kweli Babu yupo hapa chini km ilivyosemwa tutakuta tu mabaki yake, basi wakaenda kuchukua
vifaa vya kisasa kuja kupima pale chini km kuna kitu chochote kwenye mashine ikaja ikapima
ikasoma pale chini kuna kitu ikapigwa alama ya sehemu inayoonekana kuna kitu wakaanza kuchimba tena upya pale ambapo mashine imeonyesha chini kuna kitu.
Kumbe kwenye kuchimba chimba wakafika sehemu kumejengwa mfano wa chumba huko chini
kimezungushiwa zege gumu wakalipasua kwenye kupenyeza penyeza mikono wakaanza kuona km wanashika nyuzi nyuzi wale watoto wakahisi labda hizi zitakua ni nywele basi wakabomoa zaidi kwenye kubomoa wakakita kitu kigumu wakajua hapa tayari tumeufikia mwili
Wakaenda kumuita Mzee wao akaja akazama kwenye shimo kuona je kweli lile ni skeleton la mwili wa binadamu, Mzee akawaambia pasueni zaidi ili nipafikie wakapasua zaidi Mzee kukagua kweli wakakuta Mwili ulifukiwa pale chini.
Hapo ndio Mzee huyo akawa ameufikia Mwili wa Baba yake aliefukiwa ndani ya nyumba yao wenyewe tangu yeye akiwa bado mtoto mdogo na sasa ameshazeeka.
The Secrets We Bury (2025)