Nyumba kubwa kunavuja kuna leakage mahali.... Muundo wetu wa habari za siri sio air tight mark tena! Kuna mianya
Mange amekuwa the first to know figure kwenye mambo mengi sana... Ni nani anampenyezea habari nyeti kabisa? Za watu binafsi na hata nyumba kuu? Au ni wale wanajeshi mashushushu waliokuja na Obama Kisha tukawakabidhi paa letu ili waangalie usalama?
Mange amekuwa snowden wa Tanzania.. Lakini sijui Kama kwa hali ilivyo atavumiliwa sana....namkumbuka Ben pekeyake na chatu
Leo kwa habari za chini ya zulia ilitoka hati ya kumkamata pengine huko aliko lakini akainyaka kabla haijamfikia rasmi... Kama kawaida yake kawafungukia mbaya
Namkumbuka Karegeya wa Rwanda na kilichompata hotelini South Africa peke yake chumbani
Mshana ,pia inaelekea watanzania wanaumia SANA na huu utawala ,haufuati haqi,utawala unaaminisha raia kuwa maisha yamekuwa magumu sababu wapija dili na wezi wamezuiwa,hapo hapo watu walioko ndani ya utawala wanaona tafauti,maana yake ni kwamba upijaji upo isipokua kwa watu muhimu na maalum ,ndio maana Mange anapata support mpaka za ndani kabisa na anatumiwa na haohao,because ndio sehemu pekee ambayo unaweza ku demonstrate the truth na kuongea habari ambazo zinaogopesha lakini zinaukweli.
Hii inadhihirisha kuwa Tanzania bado haijakuwa kwenye mikono ya watu sahihi .Maskini ataizidi kuwa maskini ,na faqiri atazidi kuwa faqiri na tajiri atazidi kuwa tajiri.Matokeo yake ndiyo hivyo maskin na mafaqiri wanaambiwa watoke nje ya box ,bimaana ,wajiajiri kama jinsi wakuu walivyojiajiri.Very Funny !
Kwakweli Mange apewe ulinzi ,na heshima kubwa na ushirikiano mkubwa,bimaana hatupaswi kumuamini Mtu yeyote isipokuwa macho yetu na masikio yetu ,ikiwa Mange anakuja na ushahidi ulio uchi ,je ni kipi tena ambacho tunaweza kuamini zaid ya macho yetu?
Cha msingi Mange ahimarishe ulinzi wake na vile vile hizi show za kibongo wala asiende,location zake zisiwe public bisababu wale wote ambao wana maslaha katika haya,hakika hawatoacha kutafuta njia ya kufanya vitimbi na ufasiqi juu ya nafsi yake ili wananchi waendelee kudanganywa na kuaminishwa kuwa utawala huu ni wa Haqi na ni wakuondoa dhulma ,hali ya kwamba wameikumbatia dhulma Katika nafsi zao na ndimi zao na vifua vyao.