Polisi wadaiwa kupokea amri ya kumpeleka mahakamani Msanii Optter

Polisi wadaiwa kupokea amri ya kumpeleka mahakamani Msanii Optter

nadhani wale "maagizo kutoka juu" wameshamzingira mama Samia tutarajie na wasiojulikana kurejea kwa kasi na noah zao nyeusi.
Nchi hii nilichokisema wakati wa mwendazake nakirudia sasa "WAKO WAOVU WANAOZINGIRA TAASISI YA URAIS KWA MANUFAA YAO" Inashangaza mtu anaanza vizuri ghafla mambo yanabadilika!!!
 
Jeshi la polisi limeendelea na danadana zake kukwepa kumpeleka msanii Optter Mahakamani huku likiendelea kuzuia dhamana yake.

Wakili kutoka kituo cha THRDC amepeleka hati ya kimahakama kuwataka Polisi kumpeleka mchora katuni Mahakamani.

Kwa mujibu wa sakata hili, RCO wa Kinondoni ameendelea kushikilia suala la mchora katuni huyu huku akielezea kuwa anatekeleza maagizo.

Jana afisa upelelezi wa shauri hili anadaiwa kuchukua maelezo ya mtuhumiwa na jana hiyo hiyo polisi wameenda kupekua kwenye makazi ya Optter. Inadaiwa mazingira yanaonesha kuwa Polisi wamekuwa wakimlazimisha mtuhumiwa akiri makosa wanayomtuhumu nayo au la ataozea jela

Polisi kituo cha Oysterbay wanadaiwa kuendelea kutengeneza mazingira ya kuhakikisha wanaendelea kumshikilia hapo kituoni.

Baadhi ya Askari wanadai, kuna shinikizo kutoka kwa wavaa viatu wakitaka kujua msanii ametumwa na nani kuchora picha inayowasumbua wakubwa.

Tutaendelea kuwajuza kinachojiri
wekani hii katuni tuione
 
wekani hii katuni tuione
Hii hapa
Screenshot_20211002-193728_Twitter.jpg
 
Kwa polisi hawa hawakawii kusema 'huyu ni gaidi na majuzi alikuwa Somalia akijifunza mbinu za ugaidi kwa Al-shabab na amekutwa na mabomu 3 na AK-47' Hao ndio mapolisi wetu!
 
Ila hiyo katuni ni kali. Huwa nacheka sana nikiiona😄

Tukirudi kwenye mada husika, kama hakuna “due process”, basi uongozi ni mbovu na udikteta uchwara bado upo.
Turushie basi nasi hiyo katuni tufurahi.
 
Back
Top Bottom